Na Fredrick Siwale - Matukio daima APP Mufindi.
Akimsomea hukumu Hakimu mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa Mh.Sekela Kyungu alisema mshitakiwa alitenda kosa hilo februari 25 mwaka 2024 huko kijiji cha Tambalang'ombe kata na Tarafa ya Malangali wilayani Mufindi.
Kyungu aliiambia Mahakama kuwa siku ya tukio mshitakiwa alimkuta mtoto huyo mwenye umri wa miaka 8 ambaye jina lake limehifadhiwa akiwa anacheza na wenzake na kumburuza hadi kichakani ambako alimfanyia ukatiri huo.
Upande wake Mwendesha mashitaka wa Serikali Ahmad Magenda aliiambia Mahakama kuwa mshitakiwa alishitakiwa katika kesi namba 7077 /2024 kwa mjibu wa sheria 130 (1),(2) na 131(3) kifungu 16 rejeo la mwaka 2022.
Mwendesha Mashitaka wa Serikali Ahmed Magenda aliiomba Mahakama kutoa adhabu kali kwa Mshitakiwa ili iwe fundisho kwa wengine wenye nia ya kutenda kosa kama hilo.
Aliendelea kuiomba Mahakama kutoa adhabu kali kwa Mshitakiwa kwani Wilaya ya Mufindi vitendo vya ukatili wa kijinsia ikiwepo Ubakaji na Ulawiti kwa Wanawake na Watoto vimeshika kasi na kuleta hofu kwa jamii.
Akisoma hukumu kwa Mshitakiwa Hakimu mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Mufindi Sekela Kyungu aliiambia Mahakama kuwa mshitakiwa ametiwa hatiani kwa kifungu 225 (2) mwenendo wa kesi namba 20 la 2022 fungu 161rejeo la 2022 cha adhabu kosa la kubaka na kuhukumiwa kwenda Jela kifungo cha maisha. . ......Mwisho............
0 Comments