Header Ads Widget

WAZAZI ,WALEZI PELEKENI WATOTO KUPATA CHANJO YA SURUA RUBELLA

 





Na Hamida Ramadhan, Matukio Daima App Dodoma


UZINDUZI wa kampeni ya Kitaifa ya Chanjo ya Surua na  Rubella imezinduliwa Leo Ijumaa Februari 16,2023 Jijini Dodoma na 

Kaimu Mkurugenzi Idara ya Kinga kutoka Wizara ya Afya ambaye alimwakilisha Waziri wa Afya Ummy Mwalimu Jina Dkt TUMAINI HAONGA  ambapo amewata wazazi na walezi kuwapeleka watoto wao kupatiwa chanjo hiyo  . 


Akizungumza wakati wa uzinduzi huo,uliofanyika katika viwanja vya Chinangali Park Jijini hapa Kaimu Mkurugenzi huyo amesema wazazi na walezi wawapeleka watoto wenye umri kuanzia miezi tisa mpaka 59 (chini ya miaka mitano) kupatiwa chanjo hiyo.


Amesema Chanjo hutolewa kila siku ila kampeni hufanyika kila baada ya miaka mitatu au minne.


"Niwaombe wazazi kuitumia fursa hii kuwapeleka watoto wao waweze kupatiwa chanjo kwani ni muhimu kwa watoto,"amesema Dkt Haonga.


Na kuongeza kusema "Tumepata mrejesho tangu kuanza jana kwa zoezi hili katika maeneo mbalimbali wazazi wamejitokeza kwa wingi,"amesema Dkt Haonga.


Amesema zaidi ya  watoto milioni 8.9 wanatarajiwa kupatiwa Chanjo katika vituo 7,373 katika maeneo mbalimbali nchini.


Aidha,amewataka Wakuu wa Mikoa,Wilaya na Waganga Wakuu wa Mikoa  na Wilaya kuhakikisha wanasimamia kikamilifu zoezi hilo.


Awali Mwakilishi wa Shirika Afya Duniani (WHO) Dkt William Mwengee amesema Tanzania kwa mara ya kwanza ilianza utoaji wa Chanjo ya Surua mwaka 1963.


Amesema jamii inatakiwa kuelimishwa madhara  yanayotokana na  ugonjwa wa Surua kwani wale wazazina walezi wa zamani wanajua madhara ya ugonjwa huo tofauti na Sasa hivi.


Amesema WHO itaendelea kutoa elimu ikiwemo kwa viongozi wa vijiji kuhusu umuhimu wa chanjo na kampeni iwe na mafanikio.


Kampeni hiyo ilianza jana Februari 15,2024 katika maeneo mbalimbali nchini na inatarajiwa kukamilika jumapili Februari 18, 2024.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI