Header Ads Widget

ALIYEOZESHWA MTOTO AHUKUMIWA MIAKA 3O JELA


Na Ibrahim yassin.matukio Daima App.Songwe

Mahakama ya Wilaya ya Mbozi mkoani Songwe  Leo imemhukumu   Given  Michael  Nzunda  (24) Mkulima, mkazi wa Shilanga kutumikia Kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa la Kubaka.


Mtuhumiwa alikamatwa Disemba 15, 2023 maeneo ya Shilanga, Kata ya Ihanda Tarafa ya Vwawa ambapo alituhumiwa kuozeshwa mtoto mwenye umri wa miaka 14 na kuishi nae kama mke na mume jambo ambalo ni kosa kisheria.


Akisoma maelezo ya hukumu ya kesi hiyo yenye kesi namba 40739 ya mwaka 2024 Hakimu mkazi wa Wilaya ya Mbozi Mheshimiwa Vitalis Changwe, alisema Mahakama imejiridhisha pasipo na shaka ushahidi uliotolewa na upande wa Jamhuri na kumtia hatiani mtuhumiwa kwa kosa la kubaka na kumhukumu miaka 30 jela ili iwe fundisho kwa wengine.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI