Na Thobias Mwanakatwe,IRAMBA
WATOTO 261,594 wenye umri chini ya miaka mitano katika Mkoa wa Singida wanatarajia kupewa chanjo ya kujikinga na ugonjwa wa Surua Rubella ambapo katika siku ya kwanza ya uzinduzi wa kampeni hiyo wamechajwa watoto 71,931.
Mkuu wa Mkoa wa Singida,Peter Serukamba katika hotuba iliyosomwa leo (Februari 16, 2024) kwa niaba yake na Katibu Tawala Mkoa wa Singida,Dk. Fatuma Mganga wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kitaifa ya kutoa chanjo ya ugonjwa wa Surua Rubella iliyofanyika katika Wilaya ya Iramba, amesema lengo ka kampeni hiyo ni kuwakinga watoto hao dhidi ya ugonjwa huo unaoenezwa kwa njia ya hewa na kusababisha kifo.
Amesema Mkoa wa Singida ulipata mlipuko wa ugonjwa wa Surua Rubella kuanzia Februari hadi Oktoba mwaka jana (2023) katika halmashauri za Itigi,Ikungi,Singida DC,Mkalama na Iramba ambapo watu 345 walipata ugonjwa huo.
"Ugonjwa huu unaweza kumpata mtu mwenye rika na umri wowote lakini watoto chini ya miaka mitano wapo kwenye hatari zaidi ya kupata ugonjwa huo, hivyo chanjo dhidi ya ugonjwa wa Surua na Rubella itatokewa katika vituo vya kutolea huduma za afya kwa mtoto nwenye unribwa miezi tisa dozi ya kwanza na akiwa na na miezi 18 atapata dozi ya pili," amesema Dk.Mganga.
Dk. Mganga amesema mkoa umesambaza chanjo zote dhidi ya ugonjwa wa surua Rubella hadi ngazi ya kituo cha kutolea huduma za afya na vifaa mbalimbali vya chanjo ambapo kampeni hiyo pia itatolewa kwenye shule,vituo vya mabasi na katika ofisi za vijiji na mitaa.
Katibu Tawala huyo ametoa wito kwa Wakuu wa Wilaya zote za mkoani hapa kupitia Kamati z Afya za Msingi (PHC) za Halmashauri kusimamia utoaji wa huduma za chanjo za watoto kwenye vituo vya kutolea huduma za afya na kwa njia ya Mkoba ili kuhakikisha watoto wote walengwa wanafikia asilimia 100.
Amesema halmashauri zote ziweke mpango mkakati wa kuhakikisha watoto wote waliokosa chanjo mbalimbali wanapatiwa chanjo ili kuepuka kutokea mlipuko wa magonjwa yote yanayozuilika kwa chanjo ukiwemo ugonjwa wa Surua Rubella.
"Ili mkoa uweze kufikia malengo,nahimiza wananchi wote kujitokeza kushiriki katika kampeni hii kwa kila mzazi ama mlezi kwa kuhakikisha walengwa wanapata chanjo katika kituo cha kutolea huduma za afya kilicho karibu yako,lakini pia kuhakikisha unamtaaridu jirani,ndugu,jamaa au rafiki yoyote unayemfahamu ana mlengwa ili aweze kuhakikisha mtoto walk anapata chanjo," amesema.
Aidha, Dk.Mganga amewashukuru wazazi kwa kushiriki kikamilifu zoezi hilo ambalo linaisha tarehe 19 mwezi huu (Februari) huku akiwaomba waendelee kuwapeleka watoto ambao badi hawajapata chanjo kwa ajili ya kuziweka familia zao salama.
Naye Mganga Mkuu wa Mkoa wa Singida,Victorin Ludovick amesema kuwa chanjo hii inatolewa katika halmshauri zote saba ambapo kauli mbiu ya kampeni ya Surua Rubella 2024 ni Onesha Upendo Mpeleke Mtoto Akachanje.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmshauri ya Iramba,Michael Matomora amesema kuwa Iramba pekee inatarajia kuchanja watoto 43,218 huku wakivuka malengo kwani malengo yao kwa siku wachanje watoto elfu kumi huku siku ya jana pekee ambayo ndio siku ya kwanza wamechanja watoto elf 12,089.
Mratibu wa Afya kwa Umma mkoa wa Singida Habib Mwinory amepongeza zoezi la leo kwa watu wengu kujitokeza huku akiwaomba waendelee kujitokeza hadi mwisho wa zoezi hili kwani linafaida kubwa kwa ajili ya afya za watoto wao.
MWISHO
0 Comments