Header Ads Widget

MIKOPO YA HALMASHAURI KICHOCHEO AJIRA KWA VIJANA - NZOTA

 


Na Fadhili Abdallah,Kigoma

SERIKALI imesema kuwa mikopo inayotolewa kutoka kwenye mapato ya ndani ya halmashauri za mkoa Kigoma imekuwa chachu katika kutengeneza ajira kwa vijana lakini kuchochea uchumi na biashara kwa wakazi wa mkoa Kigoma.


Katibu Tawala wa wilaya Kigoma, Mganwa Nzota alisema hayo  akizungumza katika hafla ya kukibidhi jumla ya pikipiki sita kwa vikundi viwili vya vijana na wanawake zenye thamani ya shilingi milioni 21 mikopo iliyotolewa kupitia mapato ya ndani ya halmashauri ya manispaa ya Kigoma Ujiji kupitia Benki ya CRDB katika mpango wa Imbeju.


Nzota alisema kuwa kutokana na umuhimu vijana katika kuchochea shughuli za kiuchumi serikali imeweka mkazo kwa halmashauri kuhakikisha inatenga fedha na kutoa mikopo kwa vijana kuanzisha na kuendeleza shughuli zao za kiuchumi lakini pia shughuli wanazoanzisha kuwa chachu katika kuajiri vijana wengi Zaidi.

Kwa upande wake Kaimu Meneja wa Benki ya CRDB kanda ya Magharibi, Anselm Mwenda  alisema kuwa kumekuwa na mafanikio makubwa kwa vijana kuona umuhimu wa mikopo hiyo na hivyo wengi kujitokeza na kwamba hadi sasa tangu mpango huo kuanza jumla ya maombi 855 yamepokelewa kutoka kwa vikundi vya vijana, wanawake, na walemavu kwa manispaa ya Kigoma Ujiji.


Awali Afisa maendeleo ya jamii wa Halmashauri ya manispaa ya Kigoma, Jabiri Majira alisema kuwa kwa mwaka huu wa fedha hadi sasa kiasi cha shilingi Milioni 619 zimeshatolewa mikopo kwa vikundi 66 kati yao vikundi vya vijana 15, wanawake 47 na walemavu vikundi vinne.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI