JUMLA ya watu 435 wanatarajiwa kupatiwa matibabu ya ugonjwa wa Vikope (Trakoma) kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha Mkoani Pwani
Hayo yalisemwa na Peter Kivumbi ambaye ni Meneja wa mradi wa Magonjwa yasiyopewa kipaumbele kutoka Sightsavers wakati wa uzinduzi wa mradi huo wa kutokomeza ugonjwa wa Vikope Mkoa wa Pwani kwa Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha.
Kivumbi alisema kuwa matibabu hayo yatatolewa bure sambamba na vifaa tiba na dawa ili kukabili ugonjwa huo ambao endapo mgonjwa asipopatiwa matibabu anaweza kupata upofu.
Kwa upande wake mratibu wa macho mkoa wa Pwani Dk Eligreater Mnzavas alisema kuwa ugonjwa huo wa Vikope unatokana na nzi kutokana mazingira kuwa machafu.
Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha Regina Bieda alisema kuwa mradi huo utasaidi kuwapatia matibabu wagonjwa hao na kuwapa dawa wale watakaobainika kuwa na dalili za ugonjwa huo.
0 Comments