Header Ads Widget

MBUNGE KIKWETE AKABIDHI KADI ZA BIMA YA AFYA KWA MABALOZI NA WENYEVITI JIMBONI CHALINZE

Na Scolastica Msewa, Msoga.

Naibu Waziri wa ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete amekabidhi kadi za bima ya afya 180 kwa Mabalozi wa nyumba kumi, wenyeviti wa CCM taei, makatibu wa CCM tawi na makatibu uenezi wa matawi ya CCM  wa kata ya Msoga jimbo la Chalinze mkoani Pwani ili kuwarahisishia namna ya kupata huduma za afya.

Amekabidhi kadi hizo za bima ya afya jana katika hafla fupi ya diwani wa kata ya Msoga Hassan Mwinyikondo akiwasilisha utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa kipindi cha miaka miwili ya 2012/2022 hadi 2022/2023 katika viwanja vya ofisi ya Kata ya Msoga na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa CCM ngazi ya Kata na wilaya na serikali.


Ridhiwani amesema lengo la kugawa kadi hizo za bima ya afya ni kulinda na kuthamini mchango wao mkubwa kwa CCM ikiwa ni pamoja na kuimarisha utendaji kazi wa Mabalozi hao wa Nyumba kumi, makatibu wa CCM tawi na Makatibu wa uenezi wa CCM tawi ili wawe na afya njema Kila siku pasipo kuteteleka na kiafya .


Amesema ugawaji huo wa kadi za Bima ya afya ni mpango endelevu katika kata zote za jimbo la Chalinze ili kuwasaidia Mabalozi kwani wanafanya kazi nyingi hasa kipindi hiki kuelekea chaguzi za serikali za mitaa.

Aidha Ridhiwani amewataka mabalozi hao, Makatibu wa CCM matawi na Makatibu wa Siasa na uenezi hao kutoa mshikamano kwa CCM hasa kipindi hiking tunaelekea chaguzi za serikali za mitaa ili kufanikisha ushindi wa CCM.


Mwenyekiti wa Halmashauri ambaye pia  ni Diwani kata hiyo ya Msoga Hassani Mwinyi kondo amesema CCM inawapenda na kuthamini mchango mkubwa unaofanywa na Mabalozi hao wa Nyumba kumi, makatibu wa CCM tawi na Makatibu wa uenezi wa CCM tawi ndio maana wametoa kadi hizo za afya kwao.


Aidha Diwani huyo ametoa shukrani zake kwa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa ushirikiano Mkubwa wa uletaji wa fedha za miradi ya maendeleo ambazo zimekuwa zikiwezesha utekezaji wa Ilani ya CCM kwenye jamii.



Amesema kata ya  Msoga imetekeleza Miradi yenye thamani ya Shilingi Bilioni 4 na Milioni mia sita Katika sekta mbalimbali ikiwemo Elimu, Afya  na wanampango wa kujenga Zahanati Katika kijiji Cha Msoga kutokana kilichokuwepo kupandishwa hadhi Hadi kufikia hospitali ya Wilaya.


Naye Diwani Viti maalumu tarafa ya Msoga Debora Rashidi amemshukuru Rais Dkt. Samia kwaajili ya kukamilika kwa wodi ya mama na mtoto katika hospitali ya wilaya Msoga ambapo Sasa pia huduma ya upasuaji wa mabusha na matende unafanyika hospitalini hapo.


Amesema huduma ya upasuaji wa mabusha na matende wilayani Bagamoyo ni huduma muhimu kwani kuna akinababa wanasumbuliwa na mabusha na matende wilayani humo hivyo wanahitaji kufanyiwa upasuaji ambapo Sasa huduma hiyo inatolewa hospitalini hapo.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI