NA WILLIUM PAUL., MOSHI.
WAKINA Mama wajawazito na wanachi wa kata ya Kirua Vunjo Magharibi wilayani Moshi mkoani Kilimanjaro wameondokana na tatizo la kutembea umbali mrefu kufuata huduma za afya baada mradi wa jengo la mama na mtoto pamoja na maabara katika kituo cha Afya Kirua Vunjo kukamilika.
Mradi ambao ulikuwa chini ya usimamizi wa halmashauri ya wilaya Moshi kwa fedha toka serikali kuu ambapo unatarajiwa kupunguza vifo vya kina mama vitokanavyo na uzazi, kuboresha huduma za afya ya uzazi, mama na mtoto pamoja na kupunguza rufaa za wagonjwa kwenda nje ya kituo hiki.
Hivi karibuni kituo hiki kilipokea vifaa tiba vya kisasa kutoka Bohari ya Dawa Tanzania (MSD) ikiwa ni muendelezo wa kuboresha utoaji wa huduma za Afya kwa wananchi.
Juhudi hizo zimetokana na Mbunge wa Jimbo la Vunjo, Dkt Charles Kimei kupaza sauti ndani na nje ya Bunge juu ya mahitaji ya wananchi ambao ambapo matunda yake yameanza kuonekana.
Hakika Jimbo la Vunjo tuna Madiwani na Mbunge wa kazi Mhe Dkt Charles Stephen KIMEI na kazi inafanyika. Asante Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa utekelezaji wa ibara ya 83 ya ilani ya uchaguzi ya CCM 2020 - 2025 kwa vitendo.
0 Comments