Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE
Wakati serikali ikitarajia kuendesha mchakato wa uchaguzi wa serikali za mitaa miezi michache ijayo mwaka huu taasisi ya kuzuia na Kupambana na Rushwa Takukuru mkoa wa Njombe imeonya wanasiasa watakaojiingiza kwenye vitendo vya utaoaji rushwa.
Mbele ya vyombo vya habari Kamanda wa Takukuru mkoa wa Njombe Cassim Ephrem wakati akiwasilisha taarifa ya Utendaji kazi ya miezi mitatu ya oktoba hadi Disemba amesema wanasiasa watakaotafuta madaraka kwa rushwa hawataachwa salama.
Baadhi ya wananchi mkoani Njombe akiwemo Gisbert Mgaya wanakiri kuwapo kwa vitendo vya rushwa wakati wa chaguzi mbalimbali huku wakitaka hatua kali kuchukuliwa kwa wanaofanya hivyo.
Vyama vya siasa ndivyo vinavyohusika katika michakato ya chaguzi mbalimbali ambavyo vinatuhumiwa kupitia wanasiasa wao kujihusha na vitendo hivyo.
Katibu wa siasa na uenezi wa CCM Mkoa wa Njombe Josaya Luoga amesema chama chao kina kanuni na taratibu za kuwashughulikia wale wote wanaotoa rushwa ili wachaguliwe.
Reginard Danda ni mwenyekiti wa CHADEMA Jimbo la Njombe mjini ambaye anataka Takukuru ifanye kazi kwa uhuru kwani kuna wakati inashindwa kutekeleza majukumu yake kutokana na kutokuwa huru.
Baadhi ya wanasiasa wanatajwa kuanza kutembeza zawadi mbalimbali hivi sasa zikiwemo za fedha,Nguo na Mablanketi kwa ajili ya kuwarubuni wananchi ili wawachague katika chaguzi zijazo jambo ambalo Takukuru wanapaswa kuongeza nguvu katika ufuatiliaji wa sauala hilo.
0 Comments