Header Ads Widget

PSPTB YATATHIMINI BAJETI MWAKA WA FEDHA 2023/2024

 

Na Hamida Ramadhan Matukio Daima App Dodoma

BODI ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) wamekutana kwenye mkutano wa Baraza la wafanyakazi kutathimini bajeti ya taasisi nakuangalia mikakati waliojiwekea mwaka wa fedha uliopita 2022/2023 na nusu mwaka 2023/2024.


Akiongea katika mkutano huo leo jijini hapa Mkurugenzi Mtendaji wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) Godred Mbanyi amesema wamekutana Wakuu wa Idara, Wakurugenzi na Menejiment ambapo lengo ni kuwasilisha bajeti walizopewa na utekelezaji wake uliopita wa mwaka wa fedha. 


Amesema baada ya mawasilisho ya bajeti,baraza litatoa maoni yake na uboreshaji wa mwaka ujao wa fedha. 

"Kama ikionekana utekelezaji na utendaji wa mwaka wa fedha haukuwa mzuri baraza litatoa mapendekezo ni namna gani kuweka mikakati ili waweze kufanya vizuri mwaka ujao wa fedha, "Amesema Mkurugenzi Mtendaji huyo. 


Amesema PSPTB ni sehemu mahususi waliyowekeza  katika kutengeneza mahusiano mazuri kati menejimeti na wafanyakazi na imewasaidia katika utekelezaji wa majukumu yao. 


"Kwasababu ni ukweli kwamba kila mmoja anajiona ni mmoja nani sehemu ya mikakati ya taasisi na hakuna jambo linalofanywa na menejimeti bila kupitia kwenye Chama cha Wafanyakazi au Baraza na hakuna mfanyakazi anayeona utekelezaji wa jambo lolote kwenye tasisi ni jipya kwani vyombo vyote vya ushilikishwaji vinausishwa katika kufanya maamuzi wa uwendeshaji wa taasisi, "Amesema. 

Na kuongeza kusema "Sasa tunaenda kufanya kwa njia ya TEHAMA kwani bajeti imeogezwa kwa asilimia 8.5 na ongezeko hilo ni katika kuongeza miundombinu ya KITEHAMA katika kutekeleza majukumu yetu na kwendana na kasi ya serikali," Amesema Mkurugenzi Mtendaji huyo. 


Amesema wanaamini Utekelezaji wa majukumu kwa kutumia mifumo ya TEHAMA kwani ufanisi unakuwa mkubwa na hata kwenye upande wa makosa yanakuwa madogo. 

Kwa upande wake  Mkuu wa Kitengo cha Masoko na uhusiano kwa umma (PSPTB ) amesema Wamekutana kwenye Baraza la Bodi la Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi Tanzania (PSPTB) na kuzungumza juu ya utekelezaji wa bajeti 2022/23 na kuangalia wanakwenda kufanya nini katika bajeti ya mwaka 2023/24.


Amesema wamekuwa wakitoa elimu kwa Umma na kwa wadau mbalimbali ambapo wataenda kuzungumza na wanafunzi wote wanausoma masomo ya Ununuzi na Ugavi katika mkoa wa Mwanza. 

Lakini pia ameeleza watatembelea vyombo vya habari na kutoa elimu juu ya sheria ya Ununuzi wa Umma imefikia wapi michakato mbalimbali inayosemekana inakwamisha watu kwenye ununuzi wa umma na wale wataalamu ambao wanafanya kazi bila kusajiliwa na (PSPTB) na kutafakari je waajiri waendelee kuwa nao au la na wale wenye makosa (PSPTB) sheria inasemaje na kuwajulisha umma juu Mtaala na sifa mpya katika vyuo.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI