Header Ads Widget

JUMUIYA YA WAZAZI CCM YAINGIA UBIA NA MWEKEZAJI KUENDESHA SHULE YA SEKONDARI YA KIBO..

 


NA WILLIUM PAUL, MOSHI. 


JUMUIYA ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi imeingia ubia na Mwekezaji St.Thomas Aquinas Foundation kwa ajili ya kuendeleza shule ya sekondari ya Kibo iliyopo manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro. 



Akizungumza mara baada ya kutembea shule hiyo na kuwakabidhi wawekezaji hao, Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Taifa na Mjumbe wa Kamati Kuu (MCC) Fadhil Maganya amesema kuwa lengo la kuwapa wawekezaji shule hiyo ni kuhakikisha wanaifufua na kufanya vizuri katika mitihani ya kifaita. 



Alisema kuwa, Jumuiya hiyo inalengo ya kuendelea kufufua miradi yote inayosimamiwa na Jumuiya hiyo na kutoa wito kwa Wawekezaji kuja kuwekeza katika Jumuiya hiyo. 



Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Kilimanjaro, Patrick Boisafi alisema kuwa, uwekezaji wa shule hiyo utaongeza ufanisi kwa chama na Jumuiya yake.



Naye Makamu Mwenyekiti wa Wazazi Taifa, Dogo Mabruk alitoa wito kwa walimu wanaofundisha katika shule zinazosimamiwa na Jumuiya hiyo kuendelea kufanya kazi kwa ufanisi ili shule hizo ziendelee kufanya vizuri.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI