Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake leo Jumanne
Februari 27,2024 amesema ziara hiyo pamoja na mambo mengine imelenga kusikiliza
na kutatua kero za wananchi kupitia mikutano ya hadhara katika Halmashauri
hizo.
Ameeleza kuwa kesho Februari 28, ziara yake itaanzia katika Manispaa ya
Shinyanga ambapo atafanya Mkutano wa hadhara
katika kata ya Mjini, kuanzia saa tano asubuhi na kwamba Alhamis Februari
29, kuanzia majira ya saa tano asubuhi atakuwa katika Manispaa ya Kahama.
RC Mndeme amesema Machi
mosi, 2024 atazungumza na wananchi wa Halmashauri
ya Msalala kupitia Mkutano wa hadhara
ambapo saa tano asubuhi atafanya Mkutano wa hadhara katika kata ya Kakola,
na baadaye Saa nane mchana atazungumza na wananchi wa kata ya Segese.
Ametoa rai kwa Wananchi wote wa maeneo atakayofanya ziara kuhudhuria katika mikutano ha hadhara ili waweze kuwasilisha kero zao,pamoja na kutoa ushauri na maoni.
0 Comments