Matukio Daimaapp. Mtwara
Mamlaka ya Anga Tanzania imewakaribisha wawekezaji katika usafiri wa anga kutumia uwanja wa Mtwara baada ya maboresho ya uwanja huo ambapo ndege zinaweza kutua muda wote.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Anga Tanzania Hamza Johari ameyakaribisha makampuni mbalimbali ya ndege kuanza kutumia uwanja wa ndege wa mtwara kwakuwa umekamilika.
Akizungumza wakati akikagua uwanja huo amesema kuwa kilichokuwa kimebakia ni mnara ambao kwa sasa umekamilika kwa asilimia 90.
Amesema maboresho hayo yatakuwa chachu ya wawekezaji kuona fursa na kuitumia ili kuweza kuboresha usafiri wa anga katika mikoa hii ya kusini.
“Kwasasa makampuni ya ndege yamekaribishwa kutumia uwanja wa ndege mtwara kwaajili ya kutoa huduma za usafiri wa anga kwenda maeneo mbalimbali ya nchi na nchi jirani pia ambapo tumetumia zaidi ya shilingi milioni 100 kukarabati mnara ambao umekamilika kwa sasa”amesema Johari
kwa upande wake Mwakilishi wa Meneja wa Kiwanja cha Ndege Mtwara Selestine Kambona amesema kuwa mnara huo ni muhimu kwakuwa ndio unasaidia kuangalia usalama wa uwanja wa ndege.
“Mnara ni muhimu kwenye kiwanja cha ndege ambapo hutusaidia kuangalia usalama wa ndege ikitua na ikiondoka baada ya maboresho ya uwanja”
“Tumeongeza urefu wa mnara ambapo zamani tulikuwa barabara za kurukia ndege zenye urefu wa mita 2250 na sasa ni mita 2800 pamoja na ujenzi wa mnara wa kuongozea ndege ili kukidhi mahitaji ya maboresho ya uwanja mpya ambapo ndege kubwa pia zinaweza kutua lakini pia usalama umeongezeka zaidi” amesema Kambona
0 Comments