Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE
Halmashauri ya mji wa Makambako mkoani Njombe imeelekeza wananchi kuanza kuchukua hatua ya kufanya matengenezo madogo madogo ya barabara hasa kufukia mashimo kutokana na miundombinu mingi kuharibika vibaya kiasi cha kukatisha mawasiliano.
Agizo hilo linatolewa na mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Makambako Hanana Mfikwa katika kikao cha baraza la madiwani cha Robo ya pili ya mwaka wa fedha wa 2024/2025 Ambapo amesema hali ya barabara kwa sasa ni mbaya sana na Tarura hawatengenezi.
Baadhi ya wawakilishi wa wananchi wa kata mbalimbali ambao ni madiwani akiwemo Iman Fute na Odilo Fute wamekiri kupokea maelekezo ya mwenyekiti wao ya kwenda kuwaelekeza wananchi juu ya ukarabati wa barabara hizo huku wakiwataka Tarura kuacha kusalia ofisini katika kipindi hiki.
Mhandisi Sikitu Pella kwa niaba ya meneja wa Tarura Makambako amesema kwa sasa mvua zimesababisha kusitisha shughuli za ujenzi na kwamba pindi zitakapopungua kazi zitaendelea.
Katika kipindi hiki cha masika hali ya miundombinu ya barabara imekuwa mbaya na kusababisha mkwamo wa shughuli za uchumi kwa wananchi.
0 Comments