NA WILLIUM PAUL, MOSHI.
MBUNGE wa Jimbo la Moshi vijijini Profesa Patrick Ndakidemi ametembelea Familia ya Balthazar Kimati, mkazi wa kijiji cha Maua kata ya Kibosho kati mkoani wa Kilimanjaro ambaye aliunguliwa na nyumba na vitu vyote vilivyokuwemo mnamo usiku wa kuamkia Februari 20 mwaka huu.
Katika ajali hiyo ya Moto, Kimati na familia yake walitoka salama ila walipoteza mali zote ikiwemo mifugo yote, pamoja na vyakula na Mali zilikuwemo ndani.
Mbunge alienda kutoa pole kwa familia hiyo kwa kufikwa na janga hilo na kuwashukuru majirani kwa ushirikiano waliounyesha kwenye kumwokoa Kimati na familia yake.
Mwisho..
0 Comments