Header Ads Widget

RAIS SAMIA MGENI RASIM MKUTANO BARAZA LA MICHEZO YA MAJESHI DUNIANI

 




Na Hamida Ramadhan Matukio Daima  App Dodoma

RAIS wa Tanzania Dkt, Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye Mkutano wa 79 wa Baraza la Michezo ya Majeshi duniani ambapo jumla ya wageni 300 kutoka nchi . 

Hayo yamesemwa leo jijini hapa na Meja Jenerali ambaye pia ni Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi wa Baraza la Michezo ya Majeshi Duniani kitoka Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) Francis Mbindi alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari juu ya mkutano huo ambapo amesema nchi wanachama 140 kushiriki mkutano huo. 


Amesema Baraza hilo lilianzishwa mwaka 1945 linaumuhihgimu mkubwa kwani lengo ni kukutanisha shughuli za Michezo na utimamu wa kimwili badala ya kutumia Vita. 


" Dhima ni Nchiwanachama kukutana katika viwanja vya Michezo kuimarisha ushirikiano badala ya kukutana kwenye viwanja vya vita, "Amesema . 


Na kuongeza" Kwani ni Tanzania tulumbuke Bara la Afrika kuna nchi 47 ambapo miongoni wa nchi hizo Tanzania imechaguliwa baada ya kukidhi kisheria, kikanuni, hali ya amani, ulizi na usalama ndivyo vigezo nchi yetu kuaminiwa , " Amesema 


Amesema mkutano huo wa siku saba ambapo utaanza rasmi tarehe 12 Mei hadi 19  Mei 2024 ambapo washiriki wa mkutano huo watatembelea vivitio vya utalii vilivyopo hapa nchini.


" Kwakuwa Mkutano huu ni wa kijeshi basi maeneo yote yaliotoa mchango wa nchi kupata Uhuru yatatembelewa ukiwemo Mnara wa mashujaa uliopo Mnazi mmoja Jijini Dar es salaam,"amesema


Na kuongeza" Ujio wa wageni utakuwa na fursa kwani nchi na jeshi litajulikana kupitia maeneo mbalimbali kiuchumi, kisiasa na kijamii na Kutangaza lugha ya kiswahili kwani katika mkutano huo jumla ya lugha tano zitatumika zikiwemo Lugha ya Kingereza, Kispania, kifaransa kiarabu na kiswahili chenyewe, " Amesema. 


Aidha amesema mwaka 1991 Tanzania iliwahi kuwa mwenyeji na mkutano ulifanyika Jijini Arusha ambapo washiriki waliweza kutembelea Mbuga za wanyama zilizopo Jijini Arusha. 


" Matarajio yetu ujio wa wageni wetu utakuwa wa manufaa makubwa kama ilivyokuwa 1991 , " Amesema


Hata hivyo katika Mkutano huo kauli mbiu unasema " Urafiki Kupitia Michezo  na utafungwa tarehe 17 na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa. 


Mwisho

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI