Mbunge wa Kalenga Jackson Kiswaga amekabidhi msaada wa saruji 50 zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni moja kwa ajili ya kuunga mkono jitihada za wananchi wa Kijiji cha ugwachana katika ujenzi wa zahanati.
Akiwa katika ziara za jimbo, mbunge Kiswaga amesema alitoa ahadi hiyo mwaka jana baada ya kuonyeshwa ujenzi zahanati hiyo, na kuwataka wananchi hao kuendelee na ujenzi huku wakitarajia kupokea misaada mingine kutoka kwake.
Pia Mbunge Kiswaga amesema malengo yake kwa sasa ni kuhakikisha mwaka huu anakamilisha ahadi zote ambazo alihahidi kwa wapiga kura wa jimbo la kalenga.
Kwa upande
wao wakazi wa Kijiji cha ugwachanya jimbo la Kalenga wamempongeza mbunge wao kwa kutekeleza
ahadi zake kwa wakati na kusema kuwa kukamilika kwa zahanati hiyo kuwapunguzia gharama
za kusafiri umbali mrefu ili kufuata huduma za afya.
Naye mtendaji wa kata ya Mseke, Wiston Muhehe, ameishukuru ofisi ya mbunge kwa kuendelea kuunga mkono jitihada za wananchi katika juhudi mbalimbali za maendeleo, na kusema kuwa mbunge huyo amekuwa akitoa misaada katika maeneo mbalimbali ya jimbo hilo.























0 Comments