Na SHEMSA MUSSA,KAGERA MULEBA ,
Serikali Wilayani Muleba Mkoani Kagera imewasisitiza Wafanyabiashara kuendelea kutekeleza na kufuata maelekezo ya Serikali kuhusiana na upandaji wa bei ya Sukari unaoendelea kuwaumiza Wananchi.
Kauli hiyo ilitolewa na Benjamin Mwikasyege ambaye ni katibu Tawala wa Wilaya Muleba kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya hiyo wakati akitoa maelekezo ya Serikali katika kikao cha Baraza la Madiwani kilicholenga kujadili taarifa za utekelezaji kwa robo ya pili Oktoba-Desemba 2023/2024 kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo.
Mwikasyege alisema kuwa katika maeneo mbali mbali sukari imepanda ambapo wao walivyokubaliana kati ya Serikali ya Wilaya hiyo na Wadau mbali mbali ni kwamba kilo moja ya Sukari iuzwe kwa kiasi cha shilingi 3,500 na kuwa katika maeneo mengine sukari imeendelea kuuzwa zaidi ya kiwango tajwa jambo linalowaumiza Wananchi na kuwa kero.
Aidha Kufuatia hali hiyo ameahidi kuwa Serikali Wilayani humo itaendelea kufuatilia jambo hilo kwa ukaribu sana ili lisiendelee kuwa kero
Hata hivyo aliwasihi madiwani wa Halmashauri hiyo kuendelea kusisitiza suala hilo kwa wafanyabiashara ili bei isizidi kiwango kilichoelekezwa na Serikali.
0 Comments