Header Ads Widget

MAREKANI YAKABIDHI KOMPYUTA 80 KWA SHULE ZA SEKONDARI NNE CHALINZE

 

Na Scolastica Msewa, Chalinze

Naibu Waziri Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete amepokea msaada wa Kompyuta Mpakato 80 zenye thamani ya Shilingi million 71 zilizotolewa na Shirika lisilo la kiserikali la  Reneal International Education Outreach la Nchini Marekani kwa ajili ya Shule nne za sekondari  zilizopo katika Halmashauri ya Chalinze.


Akizindua mradi wa matumizi ya  Kompyuta hizo mpakato katika makabidhiano ya vifaa vya mradi wa kompyuta (TEHAMA) kwa shule nne za sekondari za Halmshauri ya Chalinze hafla iliyofanyika katika shule ya Sekondari ya Mboga ambayo imekabidhiwa kompyuta mpakato 20.


Ridhiwani Kikwete amesema kompyuta hizo zinakwenda kurahisisha upatikanaji wa taarifa za masomo na kuwezesha Walimu na wanafunzi kupata elimu kwa njia ya kisasa na rahisi hasa rejea ya masomo na mitihani  yote ya taifa ya kidato cha pili na Nne.


Amesema lengo kubwa la kuanzisha maabara za kompyuta (TEHAMA) kwenye shule za sekondari hizo ni kusaidia ujifunzaji kwa wanafunzi na kwa walimu ufundishaji wa masomo ya sekondari hususani masomo ya sayansi.



Mratibu wa shirika lisilola kiserikali la Reneal International Education Outreach na Afisa TEHAMA wa Wizara ya Habari na Mawasiliano na Technolojia ya Habari David Nyangaka amezitaja shule za sekondari zitakazonufaika na mradi huo kuwa ni pamoja na Msata, Mdaula na Mandera ambapo kila kompyuta imewekwa mitihani ya kitaifa iliyofanyika nchini kuanzia mwaka 1988 ili wanafunzi watumie kujisomea.

Amesema anatarajia kuongezeka kwa ufauli wa wanafunzi katika shule hizo hivyo amewataka kusoma kwa bidii ili kulipia fadhira ya juhudi kubwa ya kuboresha elimu nchini inayofanywa na serikali.


Aidha amewaahidi iwapo watatunza vizuri kompyuta hizo itakuwa ndio kigezo cha kuletewa kompyuta zingine ili kuendelea kutosheleza idadi ya wanafunzi na idadi ya Shule za sekondari katika Halmshauri hiyo ya Chalinze.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI