Header Ads Widget

ACT WAZALENDO YAKAA MGUU SAWA UCHAGUZI MKUU NDANI YA CHAMA

 

Mwenyekiti wa Kamati ya Chaguzi ACT WAZALENDO, Joran Bashange akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) Leo jijini Dar es Salaam kuhusu kukamilika kwa mchakato wa urejeshaji wa fomu za uchaguzi ndani ya chama hicho.

xxxxxxxxxx

NA ARODIA PETER,MATUKIO DAIMA App- DAR

Chama cha ACT Wazalendo sasa kipo mguu sawa kwa Uchaguzi Mkuu wa ndani ya chama kwa mujibu wa ratiba ya chama hicho.


Taarifa ya Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi, Joran Bashange kwa waandishi wa habari leo Februari 25.2024 imesema; pazia la urejeshaji wa fomu za uchaguzi wa ndani ya chama ngazi ya taifa umekamilika.


Amesema mchakato wa uchaguzi ngazi ya Taifa ulikuwa umefunguliwa pazia la kuchukua na kurejesha fomu kuwania nafasi mbali mbali za chama na Ngome zake. Na kwamba ugawaji wa fomu hizo ulikuwa unafanyika mikoa yote na majimbo yote nchi nzima.


"Leo tumewaita kuwaeleza kuwa pazia la uchukuaji na urejeshaji fomu limefungwa jana tarehe 24 Februari, 2024 saa 10.00 jioni.


"Hivi sasa Kamati Maalum ya Uchaguzi Taifa, inaendelea na uchambuzi wa fomu za wagombea ili kuziwasilisha kwenye mamlaka za uteuzi tayari kwa uchaguzi."amesema Bashange na kuongeza kuwa;


"Kwa mujibu wa Daftari la Wapiga Kura la Chama, Mkutano Mkuu wa chama unatarajiwa kuwa na wapiga kura takriban 687, na Mikutano Mikuu ya Ngome wajumbe 132 kila mmoja (jumla 396).


Aidha "Kamati ya Uchaguzi inapenda kusisitiza kuwa mpaka sasa hakuna wagombea rasmi kwani uteuzi kupitia mamlaka husika bado, hivyo katika kipindi kilichobakia cha kampeni, watia nia wote ni marufuku kufanya kampeni zinazokwenda kinyume na mambo yaliyokatazwa chini ya kanuni ya (4) ya Nyongeza ya Kanuni za Uchaguzi (2024) inayokataza:- 

Mgombea kutoa rushwa ya aina yoyote kwa wapigakura;

Mgombea kutoa lugha ya matusi au ya kuudhi dhidi ya mgombea mwenzake.amesisitiza Bashange ambaye pia ni Naibu Katibu mkuu Bara wa chama hicho.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI