Na Scolastica Msewa, Chalinze
Naibu Waziri wa ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Chalinze Mheshimiwa Ridhiwani Kikwete amepokea na kuzindua Mradi wa Umeme wa Sola katika Shule ya Sekondari ya Jakaya Mrisho Kikwete wenye thamani ya zaidi ya milioni 16 huko Msolwa Chalinze mkoani Pwani msaada uliotolewa na Kampuni ya Matheostechs kwa lengo la kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya sita katika kuboresha sekta ya elimu nchini.
Mheshimiwa Ridhiwani amepokea na kuzindua Mradi huo wa Umeme wa Sola huko Katika shule mpya ya Jakaya Mrisho Kikwete ambayo imejengwa kwa lengo la kusogeza Shule ya Sekondari kwenye kijiji ambacho walikuwa wakitembea umbali mrefu kufuata shule.
Amesema shule hiyo mpya inayoendelea kujengwa Ina miundombinu mizuri lakini hakukuwa na umeme kwakuwa umeme hajafika katika eneo.hilo lakini kwa ushirikiano wa Kampuni ya Matheostechs wakesaidia kumaliza tatizo Hilo la kukosa Umeme shuleni hapo
Aidha amewataka Wanafunzi, Walimu na Wazazi kuisaidia kutunza miundombinu mizuri ya mfumo wa
Umeme huo sambamba na kuwataka Wanafunzi kusoma kwa bidii kwa lengo la kuenzi jina kubwa la Jakaya Mrisho Kikwete.
0 Comments