Header Ads Widget

BITEKO:TUNAANZA KUJENGA MRADI WA UMEME WA MAJI WA RUMAKALI WA MAKETE NJOMBE

 






Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE


Serikali imeahidi kuanza utekelezaji wa mradi mkubwa wa umeme wa maporomoko ya maji wa Rumakali uliopo wilayani Makete mkoani Njombe baada ya kukamilika kwa usanifu na tathmini ya mali za wananchi wanaopaswa kulipwa fidia.


Mradi huo utakuwa wa pili kwa ukubwa ukitanguliwa na ule wa bwawa la Mwalimu Nyerere uliopo Rufiji mkoani pwani ambao umefikia zaidi ya asilimia  90 katika utekelezaji wake na katika siku za usoni mtambo wa kwanza utawashwa.


Waziri wa Nishati na Naibu Waziri mkuu Dokta Dotto Biteko ametembelea katika mradi huo uliopo katika kata ya Iniho Wilayani Makete ambapo amewahakikishia wananchi kuanza utekelezaji wa mradi huo muda mfupi ujao.


Awali mratibu wa mradi huo Mhandisi Toto Ezekia anasema mradi huo wenye uwezo wa kuzalisha umeme wa megawati 222 Umefikia hatua nzuri na kuwaahidi wananchi juu ya ulipwaji wa fidia zao.


Mbunge wa Makete Festo Sanga anasema wananchi wamepisha maeneo yao kwa miaka mingi na hawaendelezi chochote pasina kulipwa fidia hivyo serikali inapaswa kuwatazama kwa jicho la karibu.


Wakazi wa Makete Ezekiel Sanga na Atupelage Sanga Wanasema hawana shida na mradi huo kikubwa walipwe fidia za maeneo yao.


Kujengwa kwa mradi huo sambamba na ule wa Ruhuji utakaozalisha umeme wa Megawatt 358 utalisaidia taifa kuwa na umeme Toshelevu na wa uhakika na kuondoa changamoto ya kukatika katika kwa umeme na kusababisha malalamiko makubwa nchini.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI