Header Ads Widget

RC SERUKAMBA: UKIUZA SUKARI BEI JUU TUTAKUFUNGULIA KESI YA UHUJUMU UCHUMI

 








Na Thobias Mwanakatwe,  SINGIDA 


MKUU wa Mkoa wa Singida,Peter Serukamba amesema mfanyabaishara yeyote atakayebainika anauza sukari kwa bei kubwa mkoani hapa kinyume na bei elekezi iliyotolewa na serikali atakamatwa na kufunguliwa mashakta ya uhujumu uchumi.


Amesema hayo leo (Februari 22,2024) baada ya kuongoza Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa kukagua maduka ya jumla yanayouza sukari mjini Singida ambapo wamebaini wafanyabiashara wanauza sukari kati ya Sh.140,000 hadi 145,000 kwa mfuko wenye ujazo wa kilo 50.



Ukaguzi huo umefanyika ikiwa ni siku moja tu baada ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mohamed Mchengerwa, kutoa agizo kwa wakuu wa mikoa kusimamia usambazaji wa sukari na kuwachukulia hatua wafanyabiashara wote wanaohujumu upatikanaji wake.


“Niwaombe ma DC kila mtu aende kwenye wilaya yake na halmashauri yake kwenye maduka yanayouza sukari kufanya ukaguzi kuomba bei za manunuzi ili kujua kama ameuzia bei ya kawaida au la kutoka kwenye maduka ya jumla na waonyeshe risiti atakayesema hana risiti huyo tumpeleke moja kwa moja tukamfungulie mashtaka  ya uhujumu uchumi,” alisema.


Serukamba alisema wafanyabiashara wote walionunua sukari kutoka kwa msambazaji mkuu wa Mkoa wa Singida watakaosema sukari imekwisha waonyeshe risiti jinsi walivyoiuza na watakaoshindwa kuonyesha risiti waingizwe kwenye kosa la kufanya biashara bila kutoa risiti.



“Mfanyabiashara atakayeshindwa kutoa risiti maana yake huyo atakuwa anayo lakini atakuwa ameamua kuificha ili auze bei kubwa huyo naye tumfungulie mashtaka ya uhujumu uchumi na wale watakaotoa ushirikiano kutoa risiti tuaangalia kwa wale waliowauzia ili tushughulike nao,”alisema.


Serukamba pia aliiagiza Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Singida ‘kuziprint’ risiti zote za wafanyabiashara wa maduka ya jumla walivyouza sukari ili kuangalia kama zinawiana na zile ambazo walipewa wafanyabiashara wa maduka ya kati na rejareja na kama itakuwa ni tofauti hatua zichukuliwe.


“Sukari itaanza kuingia, Afisa Biashara wa Mkoa hakikia unasimamia msambazji mkuu wa sukari jinsi anavyogawa sukari maana hapa tumeona anawauzia wafanyabiashara wenzake wa mjini ili nao wakalangue watu wengine wakati inatakiwa kila wilaya ipate mgao sawa,” alisema.


Naye mmoja wa wafanyabiashara wa duka la jumla, Muhsin Damji, aliishauri serikali badala ya sukari kuagizwa na wafanyabishara wachache wanaopewa vibali na serikali badala yake iruhusu kila mfanyabiashara mwenye uwezo aagize sukari hata kutoka nje  cha msingi alipe kodi ya serikali kama inavyotakiwa.


Kamati hiyo ya ulinzi na usalama wa katika ukaguzi huo uliofanyika kwenye maduka ya jumla ya Nagji, Vunja bei (Jaffa Gangij),Muhsin Damji,Shamsa Shop na Best Shop walibaini bei za sukari zinazouzwa na wafanyabiashara hao ni kati ya Sh. 140,000 hadi 145,000 kwa mfuko wenye ujazo wa kilo 50.


Naye Meneja wa TRA Mkoa wa Singida, Azaria Kasomi,alisema ukaguzi wa risiti kwenye maduka utaendelea kufanyika kuanzia leo/jana na atakayebainika hajatoa atatozwa faini ya Sh.1,500,000.


MWISHO

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI