Header Ads Widget

ASHIRIKI KWENYE KONGAMANO LA WANAWAKE KUELEKEA KILELE CHA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI

Na Mapuli Kitina Misalaba

Naibu waziri ofisi ya waziri mkuu kazi, vijana na ajira  Mhe. Paschal Patrobas Katambi amewakumbusha wanawake wote hapa Nchini kuwajibikia jukumu la malezi bora na makuzi ya watoto kama hatua ya kulinda maadili.

Katambi ambaye pia ni mbunge wa Jimbo la Shinyanga mjini ametoa kauli hiyo leo wakati akizungumza kwenye kongamano la wanawake kuelekea kilele cha siku ya wanawake Duniani.

Amesema ili kukabiliana na tishio la mmomonyoko wa maadili ni wajibu wa kila mwanamke na jamii kwa ujumla kusimamia malezi na makuzi ya watoto kwa kuzingatia maadili mema.

Katibu wa jukwaa la uwezeshaji wanawake kiuchumi Taifa Dkt. Regina Malima amewataka wanawake kuchukua hatua haraka katika kujikwamua kiuchumi huku akiwaomba kuendelea kuunga mkono juhudi za serikali katika shughuli za maendeleo.

Mwenyekiti wa jukwaa la uwezeshaji  wanawake kiuchumi Manispaa ya Shinyanga Mwalimu Zezema Shilungushela amesema jukwaa hilo limelenga kuwapataia elimu na fursa mbalimbali wanawake.

Jukwaa la wanawake Manispaa ya Shinyanga leo limefanya kongamano kuelekea siku ya wanawake Duniani Machi 8 na kwamba kauli mbiu ya mwaka huu inasema “Wekeza kwa wanawake kuharakisha maendeleo ya Taifa na ustawi wa jamii”.

Katika kongamano hilo mada mbalimbali zimetolewa na wawezeshaji ikiwemo mada ya Afya ya akili, malezi ya watoto, wanawake na uongozi pamoja na ukatili wa kijinsia.Awali baadhi ya viongozi wakisalimiana kabla ya kuingia ukumbini.

Buruduni ikiendelea katika kongamano la wanawake wa jukwaa la uwezeshaji kiuchumi Manispaa ya Shinyanga, kuelekea kilele cha siku ya wanawake Duniani.


 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI