Header Ads Widget

PUMZIKA KWA AMANI MZEE "RUKSA"


TAZAMA VIDEO YA KAULI YAKE KABLA YA KIFO

RAIS wa Serikali ya Awamu ya Pili, Mzee Ali Hassan Mwinyi, amefariki dunia wakati akipatiwa matibabu ya ugonjwa wa saratani ya mapafu, katika Hospitali ya Mzena jijini Dar es Salaam.


Kufuatia msiba huo uliotokea leo, Rais Dk. Samia Suluhu Hassan ametangaza siku saba za maombolezo ambapo bendera zitapepea nusu mlingoti.


“Rais wa Serikali ya Awamu ya Pili wa Tanzania, Ali Hassan Mwinyi, amefariki Dunia leo saa 11.30 jioni katika Hospitali ya Mzena jijiji Dar es Salaam alipokuwa akipatiwa matibabu ya ugonjwa wa saratani ya mapafu.


“Mwinyi amekuwa akipatiwa matibabu tangu Novemba mwaka jana huko London nchini Uingereza na baadaye alirejea nchini ambapo aliendelea na matibabu katika Hospitali ya Mzena hadi umauti ulipomkuta,” alieleza Rais Dk. Samia.


Aliongeza: “Kwa niaba ya Serikali ya Tanzania natoa pole kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki na Watanzania wote kwa msiba huu mkubwa. Kufuatia msiba huu natangaza siku saba za maombolezo kuanzia leo ambapo bendera zitapepea nusu mlingoti,” alisema.


Kufuatia msiba wa Mzee Mwinyi, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Januari Makamba, alisema kuanzia kesho balozi zote za Tanzania zitafungua vitabu vya maombolezo kwa muda wa siku saba kwa ajili ya kutoa fursa kwa Watanzania na marafiki wa Tanzania nje ya nchi, kutoa salamu za rambirambi.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI