Na Hamida Ramadan Matukio Daima App Dodoma
WIZARA ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kuwatangazia na kuwataka watumishi wa Serikali kuomba ufadhili wa masomo ya muda mrefu na muda mfupi yanayoyolewa na Serikali kuhusu masuala mbalimbali ya TEHAMA katika vyuo vinavyotarajiwa kujengwa vya TEHAMA.
Hayo yameelezwa leo Jijini hapa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Mohamed Khamis Abdulla wakati akizungumza na Waandishi wa habari kuhusu mashirikiano na Washauri elekezi wa Chuo Kikuu cha Hanyang cha Korea kwa kufungua rasmi maandalizi ya ujenzi wa Chuo cha TEHAMA Dodoma ambacho kitakuwa na uwezo wa kudahili wanafunzi 15,000 kwa mwaka huku upembuzi wake yakinifu utachukua miezi sita kukamilika.
Ameeleza kuwa mahitaji ya awali ya Chuo hicho, yanajumuisha aina ya majengo na masomo yatakayo fundishwa yameandaliwa na kuwasilishwa na Exim Bank.
Amesema, Serikali imeweka mpango wa ufadhili wa mafunzo ya muda mrefu na mfupi kwa watumishi wa Umma 500 kwenye kozi za kuongeza ujuzi
kwenye masuala yanayohusu TEHAMA hususani Teknolojia .
Amefafanua kuwa katika awamu ya kwanza jumla ya watumishi wa umma 20
wameweza kufadhiliwa katika mafunzo ya muda mrefu katika vyuo vikuu nje
ya nchi ambapo kozi walizoenda kuongeza ujuzi ni kwenye masuala
yanayohusu Teknolojia zinazoibukia.
Amesema wapo kwenye maandalizi ya mwisho ya kupeleka wataalamu 40 kwenye mafunzo ya muda mrefu nje ya nchi ambapo kati ya hao 15 ni Maprofesa kutoka Chuo Kikuu cha Dar- es Salaam (5), Chuo Kikuu cha Dodoma (5) pamoja na Mbeya University of Science and Technology (MUST - 5) ;
"Lengo ni kuwajengea uwezo Maprofesa hao kwenye Teknolojia zinazoibukia na
watakapomaliza waweze kuendelea kutoa mafunzo katika vyuo walivyotoka
na wakati Chuo Mahiri cha Tehama kinaendelea kujengwa, "amesema Katibu
Mkuu huyo.
Ameeleza kuwa nafasi 15 zitatolewa kwa watumishi wa Umma kutoka kwenye Taasisi ya benki ya Tanzania (BOT) watumishi watano, Mamlaka ya Mapato (TRA )watano, Akili bandia kwenye ukusanyaji wa kodi), Mamlaka ya Vitambulisho (NIDA Watano kwenye big data analytics pamoja na Akili bandia huku nafasi 10 zitatolewa kwa Watumishi wa Umma kwenda kusoma kwenyemasoma ya Anga za Juu.
"Leo hii nawatangazia Watumishi wa Umma uwepo wa nafasi 440 za ufadhili wa mafunzo ya muda mfupi kwenye masuala ya TEHAMA na Teknolojia zinazoibukia kwa Watumishi wa Umma
Wizara yangu kwa kushirikiana na
Ofisi ya Rais - UTUMISHI (OR-MUUUB) tutaendelea kuhakikisha tunasimamia mafunzo kwa kada hii ya TEHAMA kwa watumishi wa Umma, "amesema
Na kuongeza " Hivyo basi napenda kuwatangazia watumishi wote wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kuwa tumefungua dirisha la maombi hayo kupitia tovuti ya www.scholarship.go.tz." Amesema Katibu Mkuu Abdulla
Kwa upande wa timu ya Washauri elekezi inaongozwa na Prof. Taejoon Park imesema hatua hiyo imetokana na ushirikiano mzuri uliopo kati ya Tanzania na nchi hiyo na kwamba kazi hiyo itafanywa kwa ufanisi na ujuzi mkubwa kwa kipindi cha muda wa miezi sita.
Amesema, "Ujenzi wa Chuo Mahiri cha Tehama eneo la Nala Dodoma
yameanza rasmi leo tarehe 29 Januari, 2024 na itasaidia kuongeza ufanisi kulingana na mahitaji ya Tehama na kupunguza tatizo la ajira kwa vijana ikiwa ni pamoja na kuendana na mapinduzi ya viwanda Duniani ya mapinduzi ya nne, ya tano na ya sita, "amesema
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM)Profesa Lugano Kusiruka,amesema Chuo hicho kama wadau wa TEHAMA
wamefurahi kushiriki kwenye maandalizi ya ujenzi huo na kwamba utakapo kamilika itasaidia kuwainua vijana wajuzi na kukuza uchumi wa kidigitali kitaifa na kimataifa.
Amesema Rais Samia ana maono makubwa ya kuwaandaa wananchi kushiriii mapinduzi hayo hivyo UDOM kama wadau wataendeleza maono hayo kwa kusafiri pamoja katika kuijenga Tanzania yenye mapinduzi ya TEHAMA.
"Kwa kuwa na Sisi tuna ndaki ya TEHAMA tutashirikiana bega kwa bega kufanikisha maono ya Serikali kuwatayarisha wataalam watakaofundisha chuo hiki kinachoanza kujengwa ,tayari tumetenga jengo kwa ajili ya jambo hili kuwapika vijana kutafsiri maono ya Rais Samia, lengo ni kuongeza uwekezaji unaoendana na kasi ya mabadiliko ya teknolojia Duniani, "amesisitiza
0 Comments