Header Ads Widget

WITO WATOLEWA KWA MAAFISA BAJETI TAWIRI KUZINGATIA MFUMO WA PEPMIS






Mkurugenzi wa Huduma za Shirika,Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI), CPA. Harold Basinda amewataka Maafisa Bajeti kutoka Idara na Vitengo na Vituo vya Utafiti  vya  Taasisi hiyo kuhakikisha uaandaji wa  bajeti  kwa mwaka wa fedha 2024/2025 unaendana na Mfumo wa kupima Utendaji Kazi wa Watumishi wa Umma na Taasisi (PEPMIS) na Mfumo maalum wa tathimini ya hali ya Rasilimali Watu Serikalini (HR Assessment).


Akizungumza wakati wa maandalizi ya mpango  wa Bajeti kwa mwaka wa fedha 2024/2025, mjini Babati, CPA  Basinda amesema,  mfumo wa PEPMIS ndio utatumika katika kupima utendaji kazi wa mtumishi mmoja mmoja, kuzipima Idara na  Vitengo, Kurugenzi,  Vituo vya Utafiti pamoja na Taasisi kwa ujumla ambapo amesisitiza  ni muhimu shughuli  zitakazo bajetiwa kwa mwaka wa fedha ujao kuendana na mfumo huo .


Naye, Afisa Mipango wa TAWIRI, Bw. Joseph Anthony ameeleza  maandalizi  ya Mpango na Bajeti katika mwaka wa fedha 2024/2025 yanazingatia Mpango Mkakati wa Taasisi, vipaumbele vya kitaifa, mwongozo wa mpango na bajeti ya serikali, Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) ya mwaka 2020-2025, Mpango wa Tatu wa Taifa wa Maendeleo wa mwaka  2021/2022 hadi 2025/2026.


Ikumbukwe, Vipaumbele vya  TAWIRI ni kufanya tafiti za kimkakati  na kusambaza matokeo ya tafiti kwa wadau, kutoa huduma za ushauri zinazohusu masuala ya uhifadhi endelevu wa wanyamapori na afya ya mifumo ikolojia ya wanyamapori nchini , kuidadi wanyamapori katika maeneo  yaliyohifadhiwa nchini, Ujenzi wa Jengo la Makao Makuu na Ukarabati wa miundombinu chakavu ya Taasisi, Kujenga uwezo wa Taasisi kuendelea  kutoa huduma na kuboresha mfumo wa ukusanyaji mapato, Kusimamia na kuimarisha miundombinu na mifumo ya TEHAMA / Teknolojia zinazohusu tafiti za wanyamapori.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI