Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Jiji Dkt.Sebastian Pima
Mwenyekiti wa Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii (CHWS) Nyamagana Yohana Wanga
Katibu Tawala Wilaya ya Nyamagana Thomas Salala
xxxxxxxxx
NA CHAUSIKU SAID, MATUKIO DAIMAAPP MWANZA.
Wananchi wa Jiji la Mwanza wametakiwa kuchukua tahadhali dhidi ya mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu baada ya kubaini wagonjwa saba wakiwa na ugonjwa huo.
Akizungumza katika kikao cha Kamati ya Afya ya Msingi ya Halmashauri hiyo Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Jiji hilo Dkt.Sebastian Pima ameeleza kuwa Januari 4 mwaka huu walipokea watu wawili waliokuwa na dalili za ugonjwa wa kipindupindu ambao walitokea Mkoa wa Simiyu.
Pima ameeleza kuwa walipata taarifa ya visa viwili baade viliendelea kutokea visa vingine eneo la Mkolani visa viwili lakini visa vitatu vinatokea Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela.
“Tangu Januari 4 mwaka huu tulipo pata mlipuko wa kipindupindu tumeisha pata wagonjwa saba ambao walilazwa ambapo wawili wa awali tumeisha waruhusu hali zao zinaendelea vizuri na kwenye kituo chetu na matibabu kwa sasa tuna wagonjwa watano ambao wanaendelea na matibabu na wanaendelea vizuri,” ameeleza Dkt.Pima.
Pima amefafanua kuwa mpaka sasa wamefanya ufuatiliaji kwa familia waliokutana na wagonjwa kwa watu 18 ambao mpaka sasa hawajaonesha dalili za ugonjwa huo na wanaendelea kuwabaini wengine zaidi kwani wagonjwa hao wamekutana na watu wengi tofauti tofauti.
“Kwa ambao wataonekana na dalili tutawachukua sampuli na wakithibitika kuwa na ugonjwa tutawachukua kwa ajili ya kuanza kuwapa matibabu " Amesema Pima.
Hata hivyo ameeleza kuwa ugonjwa huo unaambukizwa kwa njia ya kula chakula,kunywa maji au kitu chochote kilichokutana na vimelea vya ugonjwa wa kipindupindu na mara nyingi unakuwa na mchanganyiko wa kinyesi chenywe vimelea.
“Tunahamasisha jamii kunawa mikono kwa maji safi yanayo tiririka na sabuni wakati wote akitoka kujisaidia,akitaka kula chochote,wakati wote wale chakula cha moto na kuepuka kula chakula kilicho poa,kunywa maji yaliochemshwa au kutibiwa kwa kuwekewa dawa,”ameeleza Dkt.Pima.
Kwa upande wake Katibu Tawala Wilaya ya Nyamagana Thomas Salala kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya hiyo, ameeleza kuwa maeneo ya shule,taasisi na masoko kuwe na wataalamu maalumu ambao wataenda katika maeneo hayo ili kutoa elimu na kudhibiti uchafu pamoja na kuweka sehemu ya kuweka taka pamoja na maji safi na salama yanakuwepo ili kuikinga jamii na mlipuko wa ugonjwa huo.
Thomas ameeleza matumizi sahihi ya vyoo,uuzaji wa vyakula holela maeneo maeneo yasiyo rasmi uthibitiwe udhibitiwe pamoja na kutoa elimu kwa jamii na kuhamasisha ili iweze kuzingatia usafi na kanuni za afya.
“Eneo la Buhongwa linapaswa kuangaliwa kwa umakini na kuhakikisha pamoja na kufanya biashara ila pawe na utaratibu wa usafi kwani tusipo dhibithi ukanda huo ambao una muingiliano mkubwa wa watu pamoja na shule ambazo zimezunguka tutapata madhara makubwa,”kuwe na vitu vya kuweka taka na maji pia usiku.
Naye Ofisa Usafi na Mazingira wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza Desderius Polle, ameeleza kuwa mkakati walionao kwa upande wa mazingira wa kuhakikisha mazingira yote yanaimarishwa ili kukabiliana na mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu kwa kushirikiana na vikundi au kampuni za usafi katika Halmashauri ya Jiji hilo.
“Halmashauri ya Jiji la Mwanza ina kitengo cha Askari lakini kwa kushirikiana na Askari wa Jeshi la Akiba kwa ajili ya kuhakikisha wanadhibiti uchafuzi wa mazingira na wote wanaofanya biashara katika maeneo ambayo siyo rasmi,hivyo natoa rai kwa waliorudi kufanya biashara kwenye maeneo ambayo siyo rasmi warudi katika maeneo yao rasmi,”ameeleza.
Mwenyekiti wa Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii (CHWS) Nyamagana Yohana Wanga ameshauri nguvu zielekezwe shuleni kwa wanafunzi ambao wapo mama ntilie wanawauzia chakula pia taarifa hiyo iwafikie wananchi kwa haraka kwa sababu ni dharura ili wachukue hatua za kujikinga na ugonjwa huo
0 Comments