Header Ads Widget

TIC KUSHIRIKIANA NA SERIKALI KUWEKA MAZINGIRA RAFIKI KWA WAWEKEZAJI WA NDANI ILI KUNUFAIKA NA FURSA ZILIZOPO.

 


NA CHAUSIKU SAID,MATUKIO DAIMAAPP MWANZA.

SERIKALI kupitia kituo Cha uwekezaji Tanzania (TIC) imeeleza kuwa itaendelea kuweka mazingira wezeshi ya uwekezaji Kwa wawekezaji wa Kitanzania ili waweze kunufaika na fursa zinazotolewa na kituo hicho Cha TIC.

Mkurugenzi Mtendaji wa kituo Cha uwekezaji Tanzania(TIC) Gilead Teri ameyasema hayo wakati alipowatembelea baadhi ya wawekezaji wa Kitanzania Jiji Mwanza  lengo likiwa ni kuwahamasisha wawekezaji wa ndani kuendelea kuwekeza.

Teri amesema kuwa taasisi hiyo inafanya uhamasishaji wa uwekezaji ili watanzania waweze kujikita kwenye kuwekeza wa mitaji yao Nchini na kuweza kukuza kipato Cha Nchi na sio kupeleka nje.

" Hapo awali ulikuwa ukisema neno uwekezaji kitu Cha kwanza kinachomuijia mtu kichwani mwake ni wageni wanapaswa kuwekeza lakini sheria ya uwekezaji ya mwaka 2022 imepanua wigo kuhakikisha watanzania Wana nafasi mara kumi zaidi kuwa wanufaika na vivutio vya uwekezaji na kuweza kuwafikia kiurahisi zaidi katika kuwekeza Nchini kwao ukilinganisha na wageni" Amesema Teri.


Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Amos Makalla ameeleza kuwa Serikali imewekeza fedha Kwa ajili ya ufugaji wa samaki wa kisasa katika ziwa Victoria ili kuhakikisha viwanda vinafufuliwa ili kuwezesha kuchakata minofu mingi ya samaki Kwa ajili ya kusafirisha.

"Kwa hiyo nyie kituo Cha uwekezaji Tanzania TIC kuja Mwanza ni fursa Kwa wawekezaji wa ndani kuelewa serikali imeimalisha mifumo ya taarifa ya sheria ya uwekezaji pamoja kuboresha mazingira ya kupata leseni Kwa muda mchache amesema Makalla"

 Makalla ameeleza kuwa Mkoa wa Mwanza ni Mkoa wa kimkakati kutokana na kuwa Mkoa wa pili Kwa kuchangia Pato la Taifa Kwa Asilimia 7.15 ukiongozwa na Jiji la Dar- es- salaam, juhudi katika uwekezaji unahitajika kupitia sekta mbalimbali za hapa Nchini.

" Kwa hiyo Mimi nisema kuwa kituo Cha uwekezaji Tanzania bora mmekuwa na ofisini inayotembea Kuna watanzania wenye fedha lakini hawafahamu kuwa wanapaswa kusaidiwa na nyie TIC kutoka kwenu kuja huku kitawasaidia watanzania kuelewa vigezo vya mtu kuwa mwekezaji" Alisema Makalla.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Chobo Investment inayojihusisha na uchakataji na usindikaji wa nyama John Chombo ameeleza Kuwa lengo la kuwekeza katika kiwanda hicho ni kuhakikisha wanakizi mahitaji ya ndani ya Nchi ili wasiweze kutegemea nje ya Nchi.


" Masoko ya huko nje yanahitaji nyama za kutosheleza ndio maana tuna mashamba ili kuongezea uandaaji wa mifugo ambayo itakuwa sahihi Kwa mlaji ili kuweza kukizi kiwango kinachopungua" Alisema Chobo.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI