Header Ads Widget

TANESCO WATEKELEZA AGIZO LA RAIS LA UPATIKANAJI WA UMEME WA UHAKIKA KWA MIKOA YA LINDI NA MTWARA

    

Maukiodaimaapp, Mtwara, 

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limetekeleza agizo la Rais Samia Suluhu la kuhakikisha mikoa ya lindi  na mtwara inapata umeme wa uhakika ambapo tayari mitambo miwili ya kuzalishia umeme imeshafanyiwa ukarabati huku mtambo mwingine ukiletwa kwaajili ya kuimarisha  hali ya upatikanaji wa umeme kwa mikoa hiyo.


Akizungumza wakati wa kukagua eneo ambalo litawekwa mtambo huo pamoja na mitambo iliyofanyiwa ukarabati kituo cha kuzalishia umeme Mtwara Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mhandisi Gissima Nyamohanga alisema kuwa ili kukabiliana na changamoto ya umeme wanatarajia kuchukua mtambo wa umeme Ubungo na kuuleta katika kijiji cha Hiari halmashauri ya wilaya ya mtwara kwaajili ya kuzalisha umeme megawati 20.

Alisema kuwa mtambo huo utazalisha umeme kwa kutumia gesi ambapo kitakuwa kituo cha pili kuzalisha umeme ndani ya mkoa wa mtwara ili kuweza kuondokana na changamoto ya umeme ambapo wilaya ya Masasi na Nanyumbu zimetengwa na kuanza kuhudumiwa na kituo cha Pachani cha wilaya ya Tunduru.  


“Tumechagua kuufunga mtambo katika kijii cha hiari ambapo ni karibu kabisa na mitambo ya gesi asilia inayomilikiwa na Shirika la Maendeleo ya Petrol Tanzania (TPDC) ili kuturahisishia kupata huduma hiyo kwa ukaribu”

.

“Kituo hicho kipya tunatarajia kizalishe megawati 20 ambapo cha zamani kwa sasa kinazalisha megawati 21 licha ya kuwa na uwezo kuzalisha 31 tunakipugnuzia kazi kwakuondoa wilaya ya masasi na tunduru ambapo watalishwa na kituo kipya cha pachani kilichopo wilaya ya Tunduru”


kwa upande wake Meneja wa Kituo cha Kuzalisha Umeme Mkoa wa Mtwara Martin Nchimbi  alisema kuwa baada ya maagizo ya Rais Samia Suluhu wamefanya maboresho katika mtambo namba 13 na nane ambayo iko tayari na inatumika ambapo mtambo mmoja namba mbili bado haujakamilika na wanatarajia kuupokea mwezi Mei mwaka huu.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI