Matukiodaimaapp, Mtwara
Mwitikio wa wanafunzi kuripoti katika shule wilayani Tandahimba Mkoani Mtwara umekuwa mkubwa ikilinganisha na miaka ya nyuma zaidi ya wanafunzi 5500 wanatarajia kujiunga na kidato cha kwanza wilayani humo.
Akizungumza na Matukiodaima jana Afisa Elimu Sekondari Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba Sostenes Luhende aamesema kuwa katika wiki ya kwanza wanafunzi wengi wameripoti shuleni tofauti na miaka mingine.
Amesema kuwa hamasa hiyo imetokana na serikali kusogeza shule karibu na wananchi ambapo wanafunzi wengi wameweza kwenda shule kwa wakati ambapo wachache waliobakia wanaendelea kufika katika shule mbalimbali wilayani humo.
Tumepata shule mpya na zimepata usajili tayari na wanafunzi wameanza kusoma awali wanafunzi walikuwa wanapata shida wanakuwa watotoro kwakutembea umbali mrefu uwepo wa shule hiyo utaongeza hamasa ya kusoma zaidi shuleni” alisema Luhende
nae Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba baisa abdallah baisa ambaye pia ni diwani wa kata ya kitama amesema kuwa serikali imefanya jitihada kubwa za kuwezesha miundombinu ya elimu katika halmshauri yetu.
“Ipo tofatui kubwa sana kwa sasa hii halmashauri ina kata 32 tarafa 7 vijiji 143 kati hizo kata 31 zina shule na zingine zina shule mbili miongoni mwa kata zilizochelewa kupata shule ni hii kata ya Mahuta ambayo serikali ilitoa Shilingi milioni 560 ili kujenga shule hiyoambapo imebakia kata ya mkwedu ambayo ipo kwenye mchakato”
Yaani kuanzia kesho madiwani wote tunafanya ziara maalum ya kuhaammsiha wananchi wazazi na walezi kuplekea watoto shule madarasa sasa hayana vumbi yana tailes hivyo hatuoni sababu ya kushindwa kupeleka mtoto shule pia kulima mazao mbadala” alisema Baisa
Mkuu wa Shule ya Sekondari Makondeni Dunstan Komba, alisema kuwa mwitiko umekua mzuri wanafunzi wengi wamefurahi kusomea katika madarasa mapya yenye mvuto na kufanya mazingira ya mtoto shuleni kuwa rafiki. Amesema kuwa shule hiyo Ina maabala tatu za masomo ya sayansi pamoja na library ya kusomea ambayo itaongeza utulivu Kwa wanafunzi kupata fursa ya kujisomea.
“Wapo wachache ambao bado hawajaripoti yaani wapo majumbani lakini tunaamini hii yote ni kutokana na kwamba ni changamoto za shule mpya na wazazi wengi hawana mwamko tunaendelea kuhamasishana na wanafunzi na viongozi mbalimbali ili kuwezesha wanafunzi wanaotakiwa kufika katika shule hii wanafika bila tatizo”
Katika harakati za kuhakiksiha watoto wanafika shuleni Mohamed Nankondya amefika shuleni hapo na kumkabidhi binti yake kwa walimu huku akkisifu jitihada za serikali ili kuhakiksha kuwa watoto wanapata elimu stahiki katika maizingra rafiki kwao.
“Nashukuru tumejengewa shule ya sekondari tumepata ukaribu ambapo tunapunguza gharama kwa watoto wetu kusoma uwepo wake umetuhamasisha zaidi wazazi kuleta watoto wetu hapa hivi unajua shule ikiwa karibu inahamasisha zaidi watoto kusomaa lakini ikiwa mbali tunapata shida ya kuhamasisha wanafunzi kusoma” amesema Nankondya
0 Comments