Header Ads Widget

SIMBA KUTANGAZA UTALII WA ZANZIBAR

 


Klabu ya Simba imetangaza rasmi kuisadia Serikali  ya Mapinduzi  ya Zanzibar SMZ   katika kutangaza Utalii kwa kutembelea maeneo yenye Vivutio vya Utalii pamoja na kuvaa Jezi zilizoandikwa Visit Zanzibar.

Simba itaanza kuvaa Jezi zilizoandikwa Visit Zanzibar  kwenye Mchezo wao wa Pili dhidi ya Singida Fountain Gate.

"Sisi kama Klabu ya Simba tunawajibu wa kusaidia Serikali  ya Mapinduzi  ya Zanzibar kwa kutangaza  Utaliii kupitia Michezo hivyo tutatembelea maeneo ya kihistoria na kuvaa Jezi zilizoandikwa Visit Zanzibar" Mtendaji Mkuu wa Simba Iman Kajula.

"Mashindano ya Mapinduzi tumeyapata heshima kubwa ndio maana tumekuja  na kikosi kamili na tumedhamiria kuyatangaza kwa ukubwa zaidi," Iman Kajula.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI