Header Ads Widget

MBUNGE WA JIMBO LA MOSHI VIJIJINI PROF PATRICK NDAKIDEMI ASHIRIKI IBADA YA KUFUNGA MWAKA HUKO SANINGO, KIJIJI CHA MANDAKA MNONO.



Na WILLIUM PAUL, MOSHI. 

MBUNGE wa Jimbo la Moshi Vijijini Profesa Patrick Ndakidemi amewapa pole wananchi walioathiriwa na mafuriko yaliyotokea hivi karibuni katika Kitongoji cha Saningo, Kijiji cha Mandaka Mnono, Kata ya Oldmoshi Magharibi, Jimbo la Moshi Vijijini.


Akizungumza jana alipokuwa kwenye ibada ya Misa katika Kanisa la KKKT Mande Emanueli,  Mbunge Ndakidemi alieleza kusikitishwa na janga hilo lililochukua roho za wananchi wawili na kusababisha hasara kubwa ya mali katika eneo hilo. 



Baada ya kuwapa pole, aliwataka   wananchi hao kuchukua tahadhari zote muhimu kujikinga na madhara kama hayo siku zijazo. 



Katika ibada hiyo, wananchi walikuwa na zoezi la kuchangia ujenzi wa kanisa lao ambapo Mbunge Ndakidemi aliguswa na kutoa mchango wake ili kusaidia nguvu za waumini katika ujenzi huo.



Kwa upande wake, Mwinjilisti Israel Lyimo aliyeendesha ibada alimshukuru Mbunge kwa kujumuika na waumini wa kanisa hilo na kusali nao pamoja na kumshukuru kwa mchango wake wa kuendeleza ujenzi wa Kanisa lao.

Mwisho

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI