Na Thobias Mwanakatwe,SINGIDA
RAIS Samia Suluhu Hassani ametoa zawadi mbalimbali za upendo vikiwamo vyakula kwa vituo viwili vya kulelea watoto yatima na waishio katika mazingira magumu vilivyopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Singida kwa ajili ya kuukaribisha mwaka mpya 2024.
Vitu vilivyotolewa kwa vituo vya Malaika wa Matumaini na Amani Center for street Children ambavyo vimekabidhiwa na Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba kwa niba ya rais ni mchele,mbuzi,maharage,sukari,sabuni,unga wa sembe na mafuta ya alizeti.
Naye Mkuu wa Kituo cha kulelea watoto cha Malaika wa Tumaini, Sista Frola Phaustine, alimshukru Rais Samia Suluhu Hassan kwa msaada huo na kwamba ameonyesha dhahiri upendo wa dhati kwa yatima.
Phaustine alisema kituo hicho kinakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa mabweni ya kutosha kwa ajili ya watoto wanaofikia umri mkubwa na kuiomba serikali isaidie kutatua changamoto hiyo.
Akizungumza baada ya kukabidhi zawadi hizo,Serukamba alisema ni dhamira yake ya dhati ya rais kuungana na watoto yatima na waishio katika mazingira magumu mkoani Singida na anawapenda watoto wote na anaungana nao katika kusherehekea sikukuu ya mwaka mpya.
"Nipende kuwapongeza na kuwashukru masista pamoja na wadau wengine ndani ya Mkoa wa Singida kwa jitihada zao katika kuyahudumia makundi yenye uhitaji,juhudi hizi zinadhihirisha wazi kuwa wadau na jamii kwa ujumla wanavyounga mkono juhudi za serikali kuhakikisha makundi hayo yanapata afya,elimu,chakula,mavazi na malazi" alisema.
Serukamba alitoa wito kwa wadau na jamii ndani na nje ya mkoa wetu wa Singida kwa upendo kuungana na Rais Samia kuendelea kuwakumbuka wenye uhitaji wakati wote.
Naye Diwani wa Kata ya Minga, Ibrahimu Mrua, nao kupitia taasisi ya uweza wa bwana wametoa zawadi za mchele,sabuni,mafuta,unga wa ugali na ngano na maharage kwa kituo cha Malaika wa Matumaini.
Mrua alisema wametoa msaada huo kwa kutambua kuwa kumsaidia wenye mahitaji kunaleta faraja kwao na neema na kutoa wito kwa watu wengine kuwakumbuka watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu.
Kituo cha Malaika wa Matumaini kina watoto yatima 48 ambao wamekuwa wakipatiwa elimu kutokana na kituo kuwa ba shule ya awali,msingi na sekondari ambayo itaanza kutoa huduma mwaka huu 2024
0 Comments