Header Ads Widget

MIKATABA YA LIGANGA NA MCHUCHUMA KUTUPIWA JICHO NJOMBE

 

Waziri wa katiba na sheria Balozi Dokta Pindi Chana

Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAAP NJOMBE

Wizara ya katiba na Sheria imelazimika kuzulu katika miradi mikubwa ya Chuma Liganga na Makaa ya mawe mchuchuma wilayani Ludewa mkoani Njombe ukiwa ni mkakati wa  kuiendea mikataba ya kisheria itakayokuwa na tija kwa pande zote pindi majadiliano na mwekezaji mpya yatakapofika tamati.



Hivi sasa miradi hiyo mikubwa imesimama Tangu serikali ilipo lipa fidia wananchi zaidi ya shilingi bilioni 15.4 


Aidha  Serikali chini ya waziri wa Katiba na Sheria Balozi Dokta Pindi Chana imesema iko mbioni kukamilisha mazungumzo na mwekezaji wa miradi hiyo  kwa kuzingatia sheria ya mapitio na majadiliano kuhusu mikataba yenye masharti hasi ili kuhakikisha rasilimali za nchi zinatumika kuongeza pato la taifa.


Ziara hiyo iliyoifikia migodi yote ya makaa ya mawe na chuma imeambatana na Mkurugenzi wa kitengo cha uangalizi wa utajiri asilia na maliasili pamoja na Meneja wa Mradi wa Liganga na Mchuchuma kutoka shirika la maendeleo ya Taifa NDC Dr. Witness Ishuza ambaye amesema  baada ya majadiliano kukamilika wanategemea kuongeza pato la Taifa kupitia madini hayo pindi yatakapoanza kufanyakazi.


Kamishna Neema Mwanga mkurugenzi kitengo Cha uangalizi Wa utajiri Asili na maliasili toka Wizara ya Katiba na Sheria

Neema Mwanga ni  mkurugenzi kitengo cha uangalizi wa utajiri Asili na maliasili toka wizara ya Katiba na sheria ambaye anasema sheria inawataka kuhakikisha kila upande unanufaika katika miradi hiyo badala ya upande mmoja kama ilivyotaka kufanyika kwenye mikataba iliyokatishwa.


Kwa upande wake mbunge wa jimbo la Njombe mjini Deo Mwanyika amesema licha ya jitihada zote zinazofanyika na serikali lakini wakazi wa Njombe wakiwemo wachimbaji wadogo wanaomba kutazamwa kwa karibu pindi miradi hiyo itakapoanza.


Baadhi ya wananchi wa Ludewa waliopata fidia katika miradi hiyo akiwemo John Biziluka na  Raphael  Memba wameomba majadiliano hayo yafanyike kwa haraka ili miradi hiyo ianze kutekelezwa kwani habari za Liganga na mchuchuma zimekuwa za miaka mingi pasina utekelezaji.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI