Mtwara. Mkaguzi wa Polisi Dawati la Jinsia na Watoto Mkoa wa Mtwara Salma Irigo amesema vitendo vingi vya ukatili dhidi ya watoto hufanywa na wanafamilia au ndugu wa karibu, hali inayosababisha ushahidi kukosekana.
Akizungumza wakati wa maadhimisho ya wiki ya sheria mkoani Mtwara, Irigo amesema baadhi ya mashahidi hukwepa kufika mahakamani kulinda mahusiano ya kifamilia na watuhumiwa, jambo linalosababisha waathirika siyo tu kukosa haki, bali pia kuathirika kisaikilojia.
Mbele ya Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Kanda ya Mtwara Rose Ebrahim, Mkaguzi huyo wa polisi amesema kuwa watoto wengi wanafanyiwa ukatili wakiwa majumbani huku wanaohusika kufanya ukatili huo wengi wao ni wanafamilia ambapo bado hali si nzuri ndani ya jamii.
Hafla hiyo inayofanyika Mjini Mtwara pia imehudhuriwa na Majaji wa Mahakama Kuu Mtwara, Saidi Ding’oi na Martha Mpaze.
Irigo amesema kuwa jamii kutotoa ushirikiano Kwa Jeshi la Polisi Kuna kwamisha kesi nyingi.
“Wengi hawatoi ushirikiano kutokana na muhali hali ambayo inapelekea watoto wengi kuathirika kisaikologia kwakuwa wanaofanya vitendo hivyo ni watu wa karibu wakiwemo ndugu wa karibu ndio maana tumejikita kutoa elimu kwa watoto wadogo kuanzia cheke chekea” amesema Irigo
Nae Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Kanda ya Mtwara Rose Ebrahim amesema kuwa Mahakama inategemea sana Jeshi la Polisi, Magereza na Mamlaka ya Mabaara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (MMS) kwenye kesi mbalimbali hauna shaka.
Amesema kuwa kesi nyingi mahakamani huwa zinasubiri udhibitisho kutoka kwa mkemia mkuu ambapo hatujawahi kuwa na shaka na ushahidi huo kutokana na umakini na namna walivyojipanga.
“Unajua kazi yenu inatakiwa kufanyika kwa uadilifu hatunjawahi kupata shida na ushahidi kutoka kwa mkemia hasa katika kesi za jinai ikiwemo ubakaji na madawa ya kulevya” Jaji Rose
“Ofisi ya mkemia ni mdau mkubwa wa mahakama kesi nyingi za madawa ya kulevya tumekuwa karibu na nyie na kunawakati tunapata tabu kuwapata lakini hatujawahi kukwama” amesema Jaji Rose
Nae Meneja Mamlaka za Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali Kanda ya Kusini Hadija Mwema amesema kuwa vinasaba vimekuwa vikichangia kuwabaini waharifu ambapo uchunguzi hufanyika kwa umakini ili kuweza kubaini waliohusika natukio hilo.
“Huwa tunawabaini wabakaji kwenye kesi za ubakaji ambapo hupokea sampuri aliyebaka na kubakwa ambapo vinasaba huchangia kwa kiasi kikubwa kumabaini mbakaji”
“Unajua kuna eneo linaitwa whypromozone ambalo linapatikana kwa wanaume tu ambapo tunapopima huwa tunapata sampuri na kuangalia nguo za ndani na kukamilisha uchunguzi wakati mwingine huwa tunatumia hadi mashuka nguo ambapo hubaini wababakaji” amesema Mwema
0 Comments