Header Ads Widget

MAADHIMISHO YA WIKI YA SHERIA YAZINDULIWA TANDAHIMBA

Katibu Tawala Wilaya ya Tandahimba Ndugu.Rashidi Hamidu Shabani  amewasistiza wananchi kutumia Wiki ya Sheria kupata Elimu  kuhusu masuala mbalimbali ya kisheria na msaada wa kisheria kutoka kwa maafisa wa Mahakama ambao watatoa huduma hiyo kwenye maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Tandahimba.

Hayo ameyasema Januari 27,2024 wakati akizindua Wiki ya Sheria  akimwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba,  kwenye viwanja vya Mahakama ya Wilaya ya Tandahimba na kuhudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Wilaya,Watumishi,Wananchi na baadhi ya wanafunzi .

" Wananchi mjitokeze kwa wingi katika maeneo ambayo  watatoa msaada wa kisheria ili mpate elimu ya masuala mbalimbali ya Sheria kutoka kwa Maafisa wa Mahakama,Mahakama zetu zimeboresha huduma ambapo sasa zinatumia mifumo katika utoaji wa huduma mbalimbali," amesaema Katibu Tawala.

Kwa upande wake Mhe.Joseph Waruku Hakimu Mkazi.Mfawidhi Mahakama  ya Wilaya ya Tandahimba amesema  wananchi katika Wiki ya Sheria watapata fursa ya kupata Elimu ikiwa pamoja na kupata  msaada wa kisheria ,Uandishi wa Wosia,Usimamizi wa.Mirathi.na huduma mbalimbali.

Aidha amesema kuwa  maadhimisho hayo yameanza Januari 24,2024 yatahitimishwa Februari 1,2024 ambapo wananchi watapata fursa ya kuzungumza na kujadiliana na Maafisa wa Mahakama na wadau mbalimbali kwa lengo la kujifunza katika maeneo waliyotenga kutolea huduma ikiwa pamoja na Mahakama ya Wilaya ya Tandahimba. 


Kila Mwaka hapa Nchini Tanzania huadhimisha Wiki ya Sheria ambapo kauli mbiu ya Mwaka huu ni "Umuhimu wa dhana ya haki kwa ustawi wa Taifa: nafasi ya Mahakama na wadau katika kuboresha mfumo jumuishi wa haki jinai"

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI