Na Esther Machangu,Matukio Daima Moshi
Mkutano wa 26, wa mwaka wa Chama Cha akiba na kukopa Cha Walimu(MRT SACCOS) ,Moshi vijijini, umegubikwa sintofahamu Inatokana na kutokulipwa Fedha zao na Hazina kwa kipindi Cha miezi 3, ambapo kwa sasa Saccos hiyo imeshindwa kuendelea kutoa mikopo kwa Wanachama wao.
Akizungumza Desemba 11,2023 katika ukumbi wa YMCA Moshi mjini, meneja wa Chama hicho Bosco simba amesema katika mkutano huo wameileta hoja hiyo ya dharura Ili kuwapata taarifa wanachama hao kujua ni hatua gani zimechukuliwa Ili kulipwa Fedha hizo na Hazina.
Simba amesema Chama hicho kinaidai hazina kuu jumla ya shilingi Million 996.5 Takribani billion moja kwa kipindi Cha miezi mitatu, ambacho ni mwezi Juni, Oktoba, na Novemba.
"Katika kipindi Cha mwezi Juni Chama kinaidai hazina milioni 300.5 mwezi October Chama kinaidai hazina milioni 336.1 na mwezi November Chama kinadai milioni 329.8 amesema Bosco"
Aidha simba amebanisha hatua walizochukua bodi ya Chama hicho ni pamoja na kukutana na waziri wa Fedha Dr, Mwigulu Nchemba Jijini Arusha na kumuomba kulifanyia kazi swala Hilo Ili kuondoa malalamiko kwa Walimu.
" tumefanikiwa kukutana na waziri wa Fedha na alitoa maaagizo ndani ya kwa kuiandikia hazina barua ya ndani ya siku mbili Fedha hizo ziweze kulipwa lakini mpaka sasa tumekuja tena kwenye mkutano huu wa 26 wa mwaka hakuna Fedha iliyolipwa alisema Bosco"
hata hivyo meneja huyo amebanisha Changamoto nyingine inayowakabili ni pamoja na tozo ya Asilimia 2% ya Kila mwezi ya makato ya Fedha zote za wanachama endapo Chama hicho kitaitaji kupokea Fedha hizo kutoka mojakwamoja hazina kuu bila kupitia kwa Mkurugenzi Ili kuepusha Changamoto za kimfumo wa malipo ya Serikali ambazo zimekuwa zikitokea mara kwa mara.
"Tumeomba Fedha zote za makato ya mikopo,hisa,akiba,na Amana za wanachama za Kila mwezi zilipwe moja kwa moja kwenya akaunti ya Chama iliyopo katika Benki ya NMB, Tozo hiyo ya Asilimia 2% ni kubwa kuliko riba inayotozwa na Vyama vingi vya Walimu, sisi Kama Chama Cha Walimu tunatoza riba ya Asilimia 1.6 kwa mkopo wa mwezi na 10.4 kwa mkopo wa Mwaka amesema Bosco.
Hata hivyo ameongeza kuwa Mapato ya Chama kwa kipindi Cha miaka 5 iliyopita sio zaidi ya shilingi Milioni 20 kwa Mwaka hivyo makato hayo ya Asilimia 2 ni wastani wa shilingi milioni 96 kwa Mwaka ambayo ni zaidi ya faida inayopatikana endapo Chama kitaingia makataba na Hazina na itaisababishia hasara ya wastani wa shilingi milioni 70 kwa kila Mwaka.
" Sisi kama Chama Cha Walimu Moshi vijijini tumepata hasara kwa kuvunja mkataba wa mawekezo katika Benki ya NMB wa kiasi Cha shilingi milioni 550, kupata hasara ya shilingi elfu 17 kwa Kila mwanachama kwa Mwaka amesema sababu ya kuvunja mikataba hiyo ni kuwezesha wanachama kupata mikopo kwa wakati, na kuondoa adha ya Ucheleweshwaji wa kupata mikopo kwa wakati kwa wanachama"
"Chama mpka sasa kina maombi ya mkopo wa milioni 410 na kimesababisha kupoteza riba ya mikopo hiyo kwa kushindwa kuwapa Walimu mikopo, na pia kwa sasa wanachama wamepoteza kabisa Imani na Chama Chao wengi wamefuta mikopo na kwenda kujiunga na Vyama vingine amesema Bosco"
Nao baadhi ya walimu akiwemo Mwalimu Magreth Sengati, Emmanuel Matali, Na Saimon Mushi wamesema kutukoana na kadhia hiyo wanayoipata hawana budi kuandama mapaka katika ofisin za Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Ili kushinikiza kupatiwa majibu ya Adha wanayoipitia ya kukosa mikopo katika Tasisi hiyo.
"Mimi ni mmoja wa wahanga wa kukosa mkopo tusubiri ndani ya wiki moja Ili tarafa zote ziwe zimeshafanya mkutano baada ya hapo tuandamane mpaka katika ofisi za mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro tumueleze haya yanayotusibu Ili atusaidie kupata ufumbuzi, haya yatakuwa ni maandamano ya amani tunaoumia ni sisi Wanachama alisema Mwalimu Sengati"
Hata hivyo mkaguzi wa nje kutoka shirika la ukaguzi COASCO, Valeria Gabriel amewatoa hofu wanachama hao kuwa Bado Chama kipo katika hali nzuri kwani kina uwezo wa kulipa madeni yake kwani kina shilingi bilioni 13.5 zilizowekezwa katika Mali za muda mfupi,huku madeni yakiwa ni shilingi bilioni 13.3 za wanachama na tasisi mbalimbali.
" mpaka sasa Chama kina faida ya shilingi bilioni 6.6 za akiba za wanachama na zinazidi kuongezeka, amesema Valeria"
0 Comments