Header Ads Widget

KATEKISTA AHUKUMIWA KUNYONGWA HADI KUFA KWA KOSA LA MAUAJI



Mahakamani Kuu Kanda ya Iringa ambayo imefanya kikao mkoani Njombe Desemba 11, 2023 imemuhukumu kunyongwa hadi kufa Daniel Philipo Mwelango (43) ambaye alikuwa Katekista wa Kanisa katoliki #Makambako mkazi wa Makambako kwa kosa la mauaji baada ya kukutwa na hatia.


Mtuhumiwa huyo alitenda tukio hilo Februari 8, 2022 kwa kumuua Daniel Elias Myamba (43) mkazi wa mtaa wa Kahawa Makambako kesi Na MC 74/2022  katika mtaa wa Bwawani mjini Makamabako.


Hukumu hiyo imetolewa mbele ya Jaji Mhe. Said Kalunde.


Akisoma hukumu hiyo Jaji wa Mahakama kuu Kanda ya Iringa amesema Mahakama imefikia uamuzi huo baada ya kujiridhisha na ushahidi uliotolewa pasipo shaka yoyote kwamba mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo.


Jaji Kalunde amesema siku ya tukio mshitakiwa alifanya maandalizi kwa kuandaa Panga,Chuma pamoja na mifuko minne ya Kinganjaa,mifuko miwili ilikuwa kwa ajili ya kuzuia damu isisambe na miwili mingine kwa ajili kuhifadhi mwili wa marehemu.


Baada ya hapo akampiga na chuma kwenye kisogo baada ya kuona ameanguka chini na kufariki alimkata vipande viwili na kuvipaki katika mifuko ya kinganjaa ili iwe rahisi kubeba mwili huo na kwenda kuutupa mbali,baada ya kuona mke wa marehemu anapiga simu mara kwa mara kwenye simu ya Maherehemu pamoja mwenyekiti wa kigango alishindwa kuubeba mwili huo na kuamua kuondoka huku akiwa amelibeba panga na kwenda kulitumbukiza katika shimo la choo cha shule ya msingi Makambako na chuma alichotumia kumpiga nacho alikificha kwenye gata karibu na duka na yeye kutorokea Dar es Saalam.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI