NA HAMIDA RAMADHANI MATUKIO DAIMA AAP DODOMA
WITO umetolewa kwa jamii kuona umuhimu na kujifunza vitu tofauti tofauti hasa vile vya kifani hali itakayomuwezesha mtu kuwa na uelewa Mpana na kuweza kupambanua changamoto mbalimbali katika jamii.
Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni,Sanaa na Michezo, na aliyewahi kuwa Msemaji Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi wa idara ya Habari Maelezo Bwana Gerson Msigwa ameyasema hayo jijini Dodoma Mara baada ya kutunukiwa Shahada ya Umahili wa Usimamizi wa Biashashara na kuahirishwa kwa Mahafali ya 14 ya Chuo St John Dodoma .
Amesema maisha yana Mambo mengi nivyema watu kuwa na fani tofauti tofauti kama yeye alivyotoka kwenye Tasnia ya Uandishi wa Habari na kwenda katika Tasnia ya Usimamizi wa Biashashara.
Amesema kuwa, kama mtu atasalia na Jambo moja pekee anaweza kujikuta kama amejifungia katika chumba kimoja pekeake.
"Nadhani ni muhimu kujifunza vitu vingi kwasababu maisha yana Mambo mengi ukibaki kwenye Jambo moja pekee umejifungia kwenye chumba kumbe kuna fursa zingine nje ya kile ulichosomea".
Na kuongeza"Ni vizuri kubobea kwenye kitu kimoja Ila ni vizuri zaidi angalau kuvijua vitu kadhaa ili unapokutana na changamoto tofauti uwe unaweza kuzimudu na hiki ndicho ambacho Mimi nimekifanya,".
Aidha amesema aliamua kufanya kozi hii ya Umahili wa Usimamizi wa Biashashara akiamini itampa Umahili katika utendeji wake wa Kazi ili kuondokana mazoea kama wengi wanavyofanya.
"Mimi nilifanya hivi kwasababu nilihitaji Sana kusomea kozi ambayo itanipa Umahili katika utendeji wangu wa Kazi hasa kufikiria kibiashara katika shughuli zetu kwangu Mimi naona hii ni moja ya changamoto ambazo katika Utumishi Umma tunazo na wengi tunafanya Kazi kwa mazoea".
"Kozi imenifundisha kufanya Kazi kwa malengo,kuheshimu muda na kufanyakazi kwa matokeo n hili ndo Jambo kubwa nililotamani nilipate pamoja na kwamba lilikuwa nje kidogo na Uandishi wa Habari ambayo ndio hasa nyumbani kwangu,iliniongezea thamani kubwa kwenye Uandishi wangu na kuongeza thamani kubwa katika Utumishi wangu".
Pia Katibu Mkuu huyo amesema kuwa katika kozi hiyo ya Umahili wa Usimamizi wa Biashashara amejifunza kufanyakazi kimkakati,kufanya Tafiti ambalo ni Jambo muhimu katika uandishi wa Habari na Mawasiliano kwani ni lazima mtu kufanya utafiti.
"Nimepata Umahili katika Usimamizi wa Biashashara,ambapo katika Usimamizi wa Biashashara nimejifunza kufanya Kazi kimkakati,kufanya Tafiti Jambo ambalo ni muhimu katika Uandishi wa Habari na Mawasiliano kwani ni lazima watu tuwe tunafanya Tafiti".
"Kumekuwa na changamoto katika Tasnia ya Uandishi wa Habari kufanya Jambo bila Tafiti matokeo yake unafanya vitu kwa kubahatisha hivyo kozi hii imenifundisha hayo pia".
Hii ni Mahafari ya 14 tangu kuanzishwa kwa Chuo cha St John Tawi la Dodoma na jumla ya wahitimu 998 wamehitimu katika kozi mbalimbali.
0 Comments