Header Ads Widget

DKT KIMEI APONGEZA KUANZISHWA MASHINDANO YA UJIRANI MWEMA.



WILLIUM PAUL, MOSHI. 

MBUNGE wa Jimbo la Vunjo Dkt Charles Stephen Kimei adhamini jezi, mipira na zawadi mashindano ya ujirani mwema yanayoshirikisha vitongoji 14 vya kata ya Makuyuni yaliyoibuliwa na wanamichezo wa kata hiyo wakiongozwa na wazee mashuhuri.


Katika kufanikisha mashindano hayo Dkt Kimei amewezesha jezi, mipira na zawadi kwa mshindi wa kwanza shilingi milioni moja, mshindi wa pili shilingi laki tano, mshindi wa tatu shilingi laki mbili na hamsini huku mfungaji bora, golikipa bora na kocha bora nao wakiondoka na zawadi nono.



Vilevile Dkt Kimei amegawa vifaa kwa timu hizo pamoja na kushiriki uzinduzi wa mashindano hayo yanayofanyika katika uwanja wa polisi Himo.


"Nawapongeza kwa kubuni na kuratibu mashindano haya, binafsi kama mpenda michezo nimeamua kudhamini mashindano haya kwa sababu michezo ni sehemu ya mazoezi ya kujenga afya, hujenga mahusiano kwa vijana, kupiga vita vitendo vya uhalifu ikiwemo dawa za kulevya, ni fursa ya kuibua na kuendeleza vipaji vya vijana. Jambo zuri zaidi leo tumeshuhudia wameanza vizuri na watazamaji wamehudhuria wengi hii inaonesha kuwa kata ya Makuyuni na Vunjo kwa ujumla wanapenda michezo,", alisema Kimei.



Katika ufunguzi wa mashindano haya ilishuhudiwa timu ya soka ya Zilipendwa ikiifunga Saghana magoli 2-1 huku timu zote zikionesha kandanda safi. 

Mwisho.. 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI