NA WILLIUM PAUL, MOSHI.
KATIKA kuhakikisha anaboresha mazingira ya wafanyabiashara wa matunda katika stendi ya mabasi Himo wilayani Moshi, MBUNGE wa Jimbo la Vunjo, Dkt Charles Kimei amekabidhi me za 20 kwa wafanyabiashara hao ili kuacha tabia ya kupanga bidhaa zao chini.
Hatua hiyo imekuja baada ya Wafanyabiashara hao kumuomba Mbunge huyo meza hizo ili kuendelea kuboresha biashara zao na kufanya kazi katika mazingira rafiki.
Jukumu la kuhakikisha kuwa wajasiriamali wanakuwa na mazingira mazuri ya kufanyia shughuli zao lisiachwe kwa serikali pekee yake bali ili kuweza kuharakisha maendeleo yao.
Katika kuunga mkono juhudi kubwa inayofanywa na serikali ya CCM Awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ya kujenga mazingira mazuri na wezeshi kwa wajasiriamali Mbunge Dkt. Kimei ameonyesha kuunga kwa vitendo.
Akizungumza katika zoezi la kukabidhi meza hizo Dkt Kimei amesema katika mwaka huu wa fedha 2023/24 Halmashauri ya wilaya ya Moshi itafanya matengenezo ya kuiboresha stendi hiyo pamoja na serikali kukamilisha ujenzi wa barabara ya Himo - Lotima kilomita 5.87
Aidha Dkt Kimei ameeleza kwamba anamshukuru sana Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa serikali anayoiongoza kuwezesha gari la wagonjwa kwa ajili ya Jimbo la Vunjo ambalo litakabidhiwa kabla ya sikukuu ya krisimasi.
Naye Katibu wa CCM wilaya ya Moshi Vijijini, Ramadhani Mahanyu amesema chama kimeshatoa maelekezo kwa Halmashauri ya wilaya ya Moshi kuendelea kuwajengea mazingira mazuri wajasiriamali wanaoendesha biashara katika maeneo mbalimbali ikiwemo kuwapanga ili waendelee na biashara zao.
Kwa upande wa wajasiriamali wa matunda walimshukuru Dkt Kimei kwa kumpa zawadi na kumuahidi kuwa naye bega kwa bega.
Katika hatua nyingine Dkt Kimei amewezesha shilingi laki tano ya kujaza vifusi kwenye barabara ya kuingia stendi ikiwa ni ombi lililowasilishwa na viongozi wa madereva wa daladala katika stendi hiyo wakati wakisubiri utekelezaji wa mpango wa halamshauri.
Katika zoezi hili walihudhuria Mwenyekiti wa Mamlaka ya Mji Mdogo wa Himo Robert Lekule, Mtendaji wa Mamlaka ya Mji Mdogo wa Himo, Diwani wa Viti Maalum, Gladness Mbwambo, Afisa Mtendaji wa kata ya Makuyuni, Jafari Mbwambo, viongozi wa CCM kata ya Makuyuni pamoja na wajasiriamali wenyewe.
Mwisho..
0 Comments