Na Shemsa Mussa,Kagera
Baadhi ya wananchi katika Manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera wameishauri serikali kuboresha zaidi katika suala la elimu bila Malipo ili kutoa Mkanganyiko walionao.
Hayo yamesemwa na baadhi ya wananchi ambao pia ni wadau wa elimu Mkoani humo wakati wakizungumza na chombo hiki akiwemo Bw Hamidu Abdulnuru ,Bw Dauda Muhammed na Bi Husna Hussein na kusema kuwa licha ya kuwepo faida ya kuondolewa ada wamekuwa wakinunua mahitaji ya shule kwa ghalama kubwa na pia kuchanga michango shuleni pila mpangilio.
Akizungumza Bw Hamidu Abdunuru Mkazi wa kata Rwamishenye Mtaa wa kamizilente ameanza kwa kuishukuru serikali kwa kuondoa ada na kuwapunguzia mzigo tofauti na pale awali ambapo baadhi ya wazazi walikuwa wakishindwa kuwapeleka watoto shule kwa kukosa ada ila kwasasa kiwango cha wanafunzi kimeongezeka kitendo kilichoifanya serikali kuongeza Madarasa ili watoto waweze kusoma vizuri.
"Kwa wale waliokuwa wanasomesha kwa miaka ya nyuma watakuwa wanakumbuka ni changamoto gani walikuwa wakizipitia na kwa sasa naamini wameanza kupata unafuu sana japo hakuna zuri au lenye kheri likakosa changamoto amesema Bw Hamidu"
Amesema licha ya jitihada zote bado kuna changamoto japo serikali imekuwa itikoa maelekezo kuwa elimu ni bure ila bado kuna vitu vinanyoendelea vinavyowapa mkanganyiko na maswali ya kujiuliza wazazi /walezi ni elimu bure au elimu bila malipo.
"Utasikia kama ni siku za mitihani utaona mtoto anatumwa 1000 sasa mzazi yeye anahesabu jumla ya shule nzima ukilinganisha ni idadi kubwa sana mimi naona serikali iboreshe vimichango hivi vidogovidogo ili tuache kujiuliza nini maana ya elimu bila malip, na wapo maafisa elimu,waratibu wa elimu wanatakiwa wapite kila shule ,kata/ kijiji kuzungumza na wazazi ,wanafunzi namna wanavyoitekeleza sera ya elimu bila malipo na kueleza wajibu wa kila mtu ameongeza Bw Hamidu"
Ameongeza kuwa anaiomba serikali kuwachukulia hatua na sheria kwa baaadhi ya walimu wanaotumia mgongo wa Elimu bila malipo kujinufaisha wao binafsi
Nae Bw Dauda Muhammed mkazi wa kata kashai mtaa wa kilimahewa ameishukuru serikali kwa kuwepo sera hiyo na kusema kuwa katika shule za Msingi sera hiyo imakuwa ikipata nafasi ngodo katika utekerezaji baada ya walimu kuongeza matumizi na mahitaji bila mpangilio.
"Mfano kuna shule sitoitaja huko Bukoba Vijijini kila mtoto alitumwa debe la Mahindi na debe la Maharage bila kuwataarifu angalau kwa mkutano wazazi ndugu yangu alinipigia simu mimi wa huku mjini labda nitakuwa najua ,hata mimi pia mtoto wangu anasoma darasa la kwanza amewahi kufukuzwa eti apeleke 2000 za mtihani nikaenda shuleni ila sikuweza kuonana na mwalimu Mkuu na nilichogundua ulikuwa utaratibu wao tu walijiwekea na nikajiuliza kwa nini tusishirikishwe ? amesema Bw Dauda"
Aidha amesema serikali iweke utaratibu wa kuweka / kuwepo wasimamizi wenye nia njema na wachapakazi na kwa michango yote itakayotolewa kwa walimu washirikishwe wazazi hiyo itakuwa bora katika kushirikiana kwa pamoja na kuboresha sera hiyo na kukuza sekta ya elimu kwa ujumla .
0 Comments