Na. Andrew Chale, Matukio Daima App Dar
Wananchi wameaswa kuchangamkia fursa ilizopo katika Sekta ya Mkonge na kujifunza uongezaji thamani wa zao la Mkonge katika matumizi mbalimbali.
Mkuu wa Masoko wa Bodi ya Mkonge Tanzania (TSB), David Maghali ametoa wito huo Julai 3,2025 alipokuwa akizungumza na baadhi ya wananchi waliofika katika banda la bodi kujifunza kuhusu Kilimo bora cha Mkonge na faida zake na Sekta ya Mkonge kwa ujumla katika Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam (Sabasaba) yanayoendelea jijini Dar es Salaam.
“Mkonge ndiyo zao la biashara pekee lenye matumizi mengi, linaweza kutumika katika kutengeneza bidhaa kama vile mazuria, magunia, mabegi, vikapu lakini pia katika ujenzi, uundaji magari na pia mabaki ya Mkonge yanaweza kuzalisha protini inayotumika kwenye chakula cha mifugo. Haya ni baadhi tu ya matumizi kati ya mengi yaliyopo,” amesema Maghali.
Bodi ya Mkonge inaendelea kuwakaribisha wadau na wananchi kutembelea katika banda lake lililopo katika Ukumbi wa Katavi (Katavi Hall) kwenye Banda la Wizara ya Kilimo.
0 Comments