Header Ads Widget

AJALI YAUA WATU 6 HUKU 19 WAKIJERUHIWA MKOANI KAGERA



Na Shemsa Mussa,Kagera.

Watu sita wamefariki  dunia  na wengine 19 kujeruhiwa katika ajali iliyohusisha gari lenye usajili namba T 339 DBV aina ya Hiace  iliyokuwa ikitokea Izimbya Bukoba Vijijini  kuelekea Bukoba Mjini.

Tukio hilo limethitishwa na kamanda wa polisi Mkoa wa Kagera Blasius Chatanda,wakati akiongea na waandishi wa habari eneo la tukio na kusema kuwa ajali hiyo ilitokea majira saa tano na nusu asubuhi maeneo ya Kyetema katikati mwa Kata mbili za Kemendo na Bujugo Halmashauri ya Bukoba.


Kamanda  Chatanda,amesema watu walipoteza maisha papo hapo 4 huku 2 walipoteza maisha wakati wahipatiwa huduma hospital  na akiwemo watoto na huku kati ya majeruhi 19 watoto ni 4 watu wazima 15 ambao walikimbizwa katika hospitali ya Bujuna ngoma ambayo ni ya Wilaya hiyo.





Amesema kutokana hali ya majeruhi  wengi kuwa mbaya wengine wamehamishiwa katika hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Kagera Bukoba kwaajili ya kuendelea na matibabu zaidi.


Amesema chanzo cha ajali hiyo uchunguzi wa awali umebaini ni mwendo kasi dereva alipokuwa akishuka kwenye mtelemko mkali aliweka gari free (Newtro )hivyo alishindwa kuirudisha kwenye mfumo wa gia  na kugonga nguzo za umeme zilizokuwa kando ya barabara na pikipiki zilizokuwa kwenye maegesho ya barabara.


“Uzembe wa mtu mmoja  unaweza kusababisha kesho waliopata ajali kupata elemavu wa kudumu na kuwa tegemezi katika familia au jamii “alisema Kamanda wa polisi mkoa wa Kagera.


Hata hivyo kamanda wa polisi mkoani humo amewataka madereva  wazingatie sheria za usalama barabarani wanapokuwa wanaendesha vyombo vya  moto na wakiwa na abiria.


Aidha.amesema kuwa hadi sasa haijafahamika kama dereva yuko hai au amefariki amedai kuwa ikithibitika yuko hai sheria itachukua mkondo wake.


Amesema waliofariki na majeruhi walio wengi bado hawajatambuliwa hivyo amewataka wanachi kufika katika hospitali hizo kutambua ndugu zao.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI