Na Fatma Ally, Matukio DaimaApp, Dar
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) linakusudia kufutia usajili vikundi vyote vya sanaa, makampuni na mapromota ambao wanaendesha shughuli za sanaa bila kufuata kanuni na utaratibu zilizowekwa kwa mujibu wa sheria.
Akizungumza na waandishi wa habari Jana Jijini Dar es Salaam Katibu Mtendaji wa Basata Dk. Kedmon Mapana amesema kupitia sheria namba 23, ya mwaka 1984 na marekebisho ya mwak 2019 inawataka wasanii wote kabla ya kutoka kwenda nje ya nchi na wanapoandaa matamasha ndani ya nchi ni lazima wapate kibali kutoka Basata.
"Kwa mfano data zetu zinaonesha vikundi vya sarakasi, kwaya, muziki wa dansi, 4989, hawa wamekuwa wakifanya biashara bila kufuata utaratibu, vikundi hivi vimesajiliwa nchini lakini wamekuwa wakifanya shughuli hizi bila kufuata utaratu,"amesema Dkt Mapana.
Ameongeza kuwa, kuna mapromota 1545 ambao wanafanya biashara ya sanaa lakini hawawaoni wakihuisha usajili wao, hivyo ni vyema wafike Basata kwa ajilinya kuhuisha vibali vyao huku Taasisi 227 wanafanya kazi bila kufuata utaratibu wa Basata.
Aidha, amewataka wasanii ambao hadi leo hawajahuisha taarifa zao wakahuishe taarifa hizo kabla ya Disemba 30 mwaka huu ili kuepuka kufutiwa taarifa zao.
Sambamba na hayo pia Basata inakusudia kutoa vyeti maalum kama sehemu ya pongezi kwa wasanii wa kikundi cha sarakasi pamoja na wasanii wa bongo fleva kwa kutii Sheria namba 23 ya 1984 iliyofanyiwa marekebisho 2019.
"Basata ndio walezi wa wasanii wote hivyo ni lazima kila msaanii anaposafiri kwenda nchi za nje kwa ajili ya kufanya show ni lazima aje achukue kibali Basata ilu kujua taarifa za Msanii husika", amesema Dkt Mapana.
Amesema vikundi vilivyofanya vizuri katika kuomba ruhusa ni pamoja na Ramadhani Brothers na upande wa madj ni Hamad Hassan Mberwa huku wasanii wa Bongo fleva ikiwa ni Ali kiba na Nasibu Abdul (Diamond platinum).
Aidha amesema ni vyema nguvu kubwa ikawekezwa kwa wasanii wa kike katika suala zima la kuomba vibali kufanya show nje ya nchi.
0 Comments