Header Ads Widget

TRA MKOA KAGERA YAHITIMISHA JUMA LA MLIPA KODI KWA KUTOA MSAADA KATIKA KITUO CHA WATOTO YATIMA NTOMA

Na Shemsa Mussa,Kagera 

Mamlaka ya Mapato  Tanzania (TRA) Mkoani kagera wamefanya hitimisho la mlipa kodi kwa kutoa mahitaji  mbalimbali vyenye jumla ya Milioni 7  katika kituo cha watoto yatima ntoma  pamoja na  kuwashukuru  waliolipa kodi kulingana na sheria. 


 Akizungumza katika hafla ya utoaji wa msaada katika kituo cha Ntoma kilichopo kata  kanyangereko ,kijiji Butanyaibega katika Halmashauri ya Bukoba  Maneja wa Tra Mkoa wa Kagera bw Mwita Ayyubu amesema kuwa  kwa kipindi cha Robo ya 2023-2024 walikuwa na lengo la kukusanya kiasi cha shilingi bilioni 28 na mpaka sasa wamefikia asilimia 99 ya makadilio ya makusanyo hivyo kuwiwa kugawana kwa kuisaidia jamii kupitia kituo cha watoto Ntoma.


"Tumefikia asilimia nzuri na hapa tumetembelea hapa kwa ajili ya kutoa nankugawana kwa kile kidogo  tulichokipata sisi kama TRA tupo katika jamii na sisi ni jamii  hivyo kila mwaka huwa tunatoa na kurudisha kwenye jamii hasa zenye uhitaji ,amesema bw Mwita"



Naibu Mkurugenzi wa hesabu za serikali (TRA) Makao Makuu  Bw Ramadhani Sengati amesema wao ni sehemu ya jamii hivyo ni jukumu kushirikiana na jamii kwa kila jambo na  kujitoa pale wanapoona kuna uhitaji ,amesisitiza wafanyabiashara kuendelea kulipa kodi hasa kwa hiyari na kusema kuwa ili Nchi ipige hatua wadau wa maendeleo ambao ni  walipa kodi lazima walipe kodi kwa mujibu wa sheria.


Awali msimamizi wa kituo cha Ntoma kinachosimamiwa na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania  (KKKT) Sr Peninnah kaimukila amesema kituo hicho  kilianzishwa mwaka 1952  na kina jumla ya watumishi 17 waliajiliwa na kusema kuwa kituo hicho tangu kimeanzishwa kimeshahudumia jumla ya watoto 1317.


Pia amesema lengo la kuanzishwa kwa kituo hicho ni kuwasaidia watoto waliopoteza mama zao na wale waliotelekezwa mitaani ,pia amesema kituo hicho kina uwezo wa kuwahudumia watoto 30 ila kutoka na changamoto mbalimbali kwenye jamii ikiwemo vifo na kutelekezwa kituo hicho kina jumla ya watoto 42.


"Kituo hiki  kinao watoto wa kiume 24 na wakike 18 ambao jumla ni 42  na kimelazimika kuwa na idadi kubwa ya watoto kuliko uwezo wake kutokana na changamoto kuongezeka katika jamii mfano wazazi kufariki ,kupata magonjwa ya afya ya akili,kutelekezwa watoto kwenye vituo vya afya na mitaani hasa katika maeneo ya mjini,amesema Sr Kaimukilwa"


Nae  Mratibu wa kitengo cha Diakoma( KKKT)Dayosisi ya Kaskazini  Magharibi  Dkt Paschal Matungwa ameishukuru Mamlaka hiyo kwa kukiona kituo hicho cha Ntoma na kusema kuwa miaka ya nyuma walikuwa wakipata msaada kutoka nchi za nje na kwa sasa wanapata misaada kutoka kwa wadau tofauti tofauti wa ndani  na kushukuru  watu kuwa na uelewa wa namna ya kuwalea na kuwahudumia watoto hao.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI