Header Ads Widget

ZITTO AWAVAA WALIOPORA ARDHI YA WANANCHI KAGERA NKANDA

 

Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo Zitto Kabwe akihutubia mkutano wa hadhara katika kijiji cha Kagera Nkanda wilayani Kasulu mkoani Kigoma


Basilio Bukuru na Desai Kasogota wananchi wa kijiji cha Kagera Nkanda

Na Fadhili Abdallah,Kigoma

Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe amemtaka Waziri wa ardhi, Waziri wa maliasili na utalii kuwachukulia hatua maafisa wa wakala wa misitu (TFS) wilaya ya Kasulu kwa kupora ardhi ya wananchi waliyopewa na Raisi Marehemu John Magufuli kwa ajili ya kilimo na badala yake maafisa hao wamegawa maeneo hayo kwa maafisa wa serikali na kuacha wananchi wakiendelea kutaabika bila kuwa na maeneo ya kilimo.

 

Zitto alisema hayo kwenye  mkutano wa hadhara kwenye kijiji cha Kagera Nkanda wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kutembelea na kufanya mikutano katika majimbo manane ya mkoa Kigoma ambapo alisema kuwa kitendo kilichofanywa na TFS dhidi ya ardhi ya wananchi hakikubaliki.

 

Sambamba na hilo Zitto amemtaka na Waziri wa TAMISEMI kuwawajibisha viongozi wa serikali katika halmashauri ya wilaya Kasulu kwa kushindwa kusimamia suala hilo kwa manufaa ya wananchi badala yake kubariki viongozi hao na wenzao wa vyombo vya ulinzi na usalama kugawana maeneo hayo na kuwaacha wananchi wakiwa hawana maeneo ya kulima huku wakikodishwa maeneo ya kilimo kwa gharama kubwa.

 

Kabwe alisema kuwa inaeleweka kwamba kijiji hicho kimezungukwa na hifadhi ya msitu wa Makere Kusini na hakuna maeneo ya kurosha ya kilimo lakini Rais Magufuli alitoa hekari 10,000 kwa wananchi hao baada ya makelele ya muda mrefu na kwamba badala yake serikali wilaya ya Kasulu inajinufaisha kwa kukodisha eneo bila kutoa risiti ambapo  ametaka wananchi wagawiwe na kuyatumia bure kufanya shughuli zao za kilimo.

 

Awali WANANCHI wa kijiji cha Kagera Nkanda wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma wakiongea na waandishi wa habari  wameiomba serikali kuwapatia maeneo yaliyotolewa kwao na Raisi Magufuli kwa ajili ya kilimo ili kuondokana  na changamoto ya kuingia kwenye maeneo ya hifadhi au kukodi maeneo kwa ajili ya kilimo kutoka kwa halmashauri ya wilaya Kasulu kwa gharama kubwa.

 

Desai Gabriel Kasogota mmoja wa wananchi wa kijiji cha Kagera Nkanda wilayani Kasulu alisema kuwa walipiga kelele kuomba kuongezewa maeneo na Marehemu Rais Magufuli aliwaongezea hekari 10,000 lakini wameshangaa halmashauri ya wilaya Kasulu imechukua eneo hilo na kuwakodisha wananchi ambao wanalazimika kulipa 50,000 kwa hekari moja kwa msimu.

  

Akitoa ushuhuda wa changamoto ya migogoro ya ardhi katika kijiji cha Kagera Nkanda hifadhi ya msitu wa Makere Kusini, Jonifas Hamenya alisema kuwa amekuwa muhanga wa vitendo vya kihuni vinavyofanywa na viongozi wa serikali halmashauri ya Kasulu na Wakala wa Misitu (TFS) kuhusu ukodishaji mashamba ambapo alilipa shilingi 200,000 kukodishiwa mashamba hekari nne lakini hakuweza kulima licha ya kulipa pesa na kufukuzwa eneo hilo.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI