NA AMINA SAID, TANGA
Naibu Waziri wa Maliasili na utalii Mhe. Danstan Kitandula tarehe 19.11.2023 alilielekeza shirika la Hifadhi Taifa Tanzania (TANAPA) kuiunganisha Hifadhi ya Taifa Mkomanzi na utalii wanaoitembelea hifadhi hiyo.
Akiwa katika Ziara ya kikazi katika hifadhi ya Taifa Mkomanzi Wilayani Same Mkoani Kilimanjaro Mhe. Kitandula alisema "Hakuna haja ya kuachia makundi makubwa ya watalii wanaozulu Zanzibar na kuondoka wakati mmeboresha Viwanja vya Ndege hivyo ni wajibu wa TANAPA kutumia fursa na mikakati ya kuwashawishi watalii kutoka Zanzibar kuja kuwaona Faru na wale wanyama wakubwa (The big 5).
Aidha Mhe. Kitandula pia amesisitiza hifadhi hiyo yenye sifa ya kuwa na Faru kujitangaza ndani na nje ya nchi hasa katika makundi makubwa.
"Tukibahatika kuwashawishi watalii hawa tutaongeza idadi ya watalii na mapato na kufikia adhma ya Serikali kabla 2025" alifafanua Kitandula.
Naibu Waziri huyo pia alipongeza Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) kwa kazi nzuri wanayoifanya ya kuvitangaza vivutio inapelekea kuongezeka kwa watalii hata hivyo aliwataka kuongeza jitihada za kukabiliana na wanyama waharibifu wakiwemo tembo.
Afisa Mhifadhi mkuu kitengo cha Utalii Mkomanzi Happiness Kiemi alimshukuru Mhe. Naibu Waziri na kuahidi kuyafanyia Kazi maagizo yote aliyoyatoa ikiwemo utatuzi wa migogoro ya wanyama pori waharibifu
Mhifadhi Kiemi alisema kuwa hifadhi hiyo imeboresha miundombinu ya utalii ikiwemo ujenzi wa lango la kuingilia wageni pamoja na Viwanja vya ndege ili kurahisisha safari za kuingia hifadhini na kutoka
Hifadhi ya Taifa Mkomanzi ni moja wapo ya hifadhi zilizoko kaskazini mwa Tanzania ikisifika kwa kuwa na idadi kubwa ya Faru weusi na inapatikana katika mikoa ya Kilimanjaro na Tanga.






0 Comments