Header Ads Widget

RAIS SAMIA MAJAJI MAHAKIMU KUTENDENI HAKI.


Na Hamida Ramadhan, Matukio Daima Media Dodoma

MAJAJI na Mahakimu wametakiwa kuhakikisha wanalinda haki,amani na utulivu kwa mustakabali wa nchi.

Agizo hilo limetolewa na RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Samia Suluhu Hassan wakati wa  ufunguzi wa Mkutano mkuu wa mwaka wa chama cha mahakimu na majaji Tanzania (TMJA) uliofanyika jijini Dodoma.

Rais Samia amesema kuwa ni muhimu kwa watoa haki nchini kusimama kwenye msitari wa haki na kufanya maamuzi ya kutoa haki. 

Aidha amesema kuwa mahakimu na majaji wanatakiwa kusimama kwenye msitari wa haki wanapotoa haki. 

"Mie ningependa sana msimamie kiapo chenu pindi mnapoapa kuwa kusimamia haki kwa kuzingatia sheria na maadili bila hofu huba wala upendeleo na hiki ndicho kiapo chenu mnapoapishwa pale mnasema nitaisimamia kazi yangu bila hofu, upendeleo huba wala chuki haya ndo mnayoyasema nami ningependa sana mkasimamie kiapo chenu,"amesema. 

Ameeleza kuwa Dira ya maendeleo ya taifa ya Tanzania 2025/2050 imejengwa juu ya misingi ya utawala bora  amani, usalama na utulivu


"Nakama inavyosema kauli mbiu yunu ya mkutano huu kwamba jukumu la mahakama katika utoaji wa haki sasa huko tunakokwemda tunapoanza utekelezaji wa dira yetu hii mahakama au muhimili wa mahakama unanafasi muhimu katika kukenga taifa letu lenye haki, amani, usalama na utulivu", amesema

Na kuongeza " Dira hii ya 2050 inatambua kwamba utawala bora na utawala wa sheri ni msingi wa maendeleo endelevu na jambo hili haliwezekani pasi na mahakama imara iliyoaminika na wananchi wake nasi Serikali tunaelekea kujenga mahakama hii tumechukua hatua kadhaa, tutaendelea kuchukua hatua kuijenga mahakama yetu iwe mahakama imara inayotoa haki kwa wananchi,"amesema. 

Akizungumzia changamoto za watumishi wa Mahakama zilizozungumzwa na jaji mkuu wa mahakama ya Tanzania George Masaju aliwataka watumishi hao kuwa wavumilivu kwani wapo watumishi wa Idara tofauti bado na wao wanachangamoto nyingi kuliko zao. 

"wakati wewe unalia pete yako uliovaa sio nzuri mwenzio analia hana hata kidole cha kuvalia iyo pete hata pete mbaya hana jipime wewe na mtu ambaye afya yako ikiteteleka anakaenda kukitengeleza kule anakurudishia afya yako na halo yako uwe jaji bora lakini bado mazingira yake ya kazi ni magumu na stahi zake ni ndogo, tujipime hapo, "


Na kuongeza "Nikisema hivyo sisemi kuwa hatutaangalia maslahi yenu lakini twendeni polepole maendeleo ni hatua tumeanza hatua za awali nanyie mmeona tumechukua hatua kubwa za kurekebisha au kuijengea heshima mahakama yetu iwe mahakama inayoheshimika duniani sasa safari ni hatua tutakwenda polepole,"amesema  Samia. 

Aidha amesema kuwa watanzania wanamatumaini makubwa na majaji pamoja na mahakimu pia wangependa kuona wanasimamia haki,uwazi na kuzingatia misingi ya kikatiba, sheria na utu. 

"Huko maabusu huko kunamtu anafungwa kwa kesi ya kubambikiwa tu sasa injiniaringi gani imepita mahakama mpaka mtu kaenda jera kwa kesi ya kubambikiwa? akitoka anasema mimi sikuwa na kesi nilibambikiwa tu lakini nimekaa nimetoka  sasa wewe uliyepeleka ukamnyima mtu uhuru wake ukaenda ukafanya afunguwe kule jipime unajukumu gani katika hilo,"amesema. 

Kwa upande wake Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania George Masaju ametoa mapendekezo ya chama cha mahakimu na majaji ikiwemo kuboreshwa kwa maslahi ya watumishi hao na migogoro ya ardhi ihanishiwe katika mahakama za mwanzo na wikaya badala ya mabaraza ya kata na mabaraza ya ardhi hali inayoleta mkanganyiko katika kutafuta suluhu ya migogoro hiyo

Wizara ya ardhi haiwezi kushughulikia masuala hayo kwa kuzingatia masuala ya kisheria

Kwa kuzingatia changamoto zilizopo katika migogoro ya ardhi na kwa kuwa serikali ipo katika mchakato wa kufanya maamuzi kwamba mashauri yote ya migogoro ya ardhi ngazi ya kata na wilaya yasikilizwe na mahakama ya Tanzania, na Mahakama ya Tanzania tunao uwezo wa kusikiliza mashauri ya migogoro ya ardhi ipasavyo, tunaishauri serikali iharakishe mchakato wa kuwezesha mashauri yote ta ardhi yasikilizwe na mahakama kuanzia mahakama za Mwanzo, Mahakama za wilaya hadi Mahakama za juu kabisa

"Kwa upande wetu Mahakama tupo tauari kushirikiana na Wizara husika na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuandaa rasimu ya Mswada, na wapo tauari kuyachambua na kuyaainisha maeneo ya vipengele vya sheria ambavyo vitaguswa katika mabadiliko hayo.





 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI